RAIS DKT. MAGUFULI ASHUHUDIA UTIWAJI SAINI MAKUBALIANO KATI YA SERIKALI NA AIRTEL

  • Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel ya India juu ya umiliki wa hisa za kampuni Airtel Tanzania na maslahi mengine ya Tanzania kutokana na biashara ya kampuni hiyo.
  • Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ametia saini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunil Mittal ametia saini kwa niaba ya kampuni ya Bharti Aitel.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabud na Mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel Bw. Sunil Mittal wakitia saini makubaliano mapya ya ubia kati ya serikali itayokuwa na asilimia 49 na Airtel na asilimia 51 kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam
  • Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Kabudi amesema katika makubaliano hayo kampuni ya Bharti Airtel imekubali kupunguza umiliki wa hisa zake za kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kutoka asilimia 60 hadi 51 na hivyo kuongeza hisa za Serikali kutoka asilimia 40 hadi 49 bila malipo yoyote kutoka Serikalini.
  • Prof. Kabudi amebainisha maeneo mengine ya makubaliano kuwa ni Serikali kupata gawio la kila mwaka kutokana na umiliki wake wa asilimia 49 ambapo inakadiriwa itakuwa ikipata shilingi Bilioni 10, kufutwa kwa madeni yote ya kampuni ya Airtel yaliyokuwa yamefikia shilingi Trilioni 1, Bharti Airtel itatoa shilingi Bilioni 1 kila mwezi kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia Aprili 2019 ili kuonesha nia njema na Bharti Airtel itatoa shilingi Bilioni 2.3 kwa ajili ya kuchangia huduma za kijamii.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal baada ya kutiwa saini kwa makubaliano mapya ya ubia kati ya serikali itayokuwa na asilimia 49 na Airteml asilimia 51 kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019. Katikati ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi
  • Maeneo mengine ya makubaliano ni Bodi ya Wakurugenzi wa Airtel Tanzania kuundwa na wajumbe 7 ambapo Serikali ya Tanzania itawakilishwa na wajumbe 3 (akiwemo Mwenyekiti atakayeteuliwa na Serikali) na Bharti Airtel itawakilishwa na wajumbe 4, Menejimenti ya Airtel Tanzania itaongozwa na Bharti Airtel lakini Afisa Mkuu wa Ufundi atateuliwa na Serikali ya Tanzania, pande zote mbili zitashirikiana kuandaa upya nyaraka muhimu za kusaidia uendeshaji wa kampuni, pande zote mbili zitashirikiana kuongeza tija na ufanisi wa Airtel Tanzania na pande zote mbili zitashirikiana kutumia miundombinu ya Shirika la Simu Tanzania (TTCL) ikiwa kuna hoja za kibiashara.
  • Kwa upande wake Bw. Sunil Mittal amesema amefurahishwa na kufikiwa kwa makubaliano katika mazungumzo hayo na amebainisha kuwa awali aliona kuna ugumu wa kufikia makubaliano lakini baadaye alielewa kuwa lengo la Mhe. Rais Magufuli ni kuhakikisha anaweka mwelekeo mzuri wenye manufaa kwa Tanzania.

 

  • Bw. Mittal ameongeza kuwa makubaliano hayo yameandika historia mpya kwa hisa nyingi kumilikiwa na Watanzania katika kampuni ya Airtel Tanzania na kwamba anatarajia kuwa Airtel Tanzania itaendelea kufanya vizuri katika soko la Tanzania ambayo ni nchi yenye uwekezaji mkubwa wa Bharti Airtel Barani Afrika.
  • Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini makubaliano hayo Mhe. Rais Magufuli ameipongeza timu iliyoiwakilisha Serikali ya Tanzania chini ya Prof. Kabudi na timu ya Bw. Mittal kwa kufikia makubaliano hayo yaliyochukua muda wa miezi 8 na ameelezea furaha yake kuwa sasa Airtel Tanzania itaanza kutoa manufaa kwa Serikali ikiwemo gawio na maslahi mengine yanayostahili, mambo ambayo hayakufanyika kwa miaka zaidi ya 8 tangu kampuni hiyo ianzishwe hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw. Sunil Colaso baada ya makubaliano mapya ya ubia kati ya serikali itayokuwa na asilimia 49 na Airtel yenye asilimia 51 kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019.
  • Amempongeza Bw. Mittal kwa kuridhia kuongeza hisa za Serikali, kutoa shilingi Bilioni 1 kila mwezi kwa miaka 5 na kutoa mchango wa Shilingi Bilioni 2.3 ambazo ameagiza ziungane na shilingi Bilioni 1 iliyotengwa kwa ajili ya sherehe za siku ya Uhuru za mwaka 2018 (na kufanya jumla shilingi Bilioni 3.3) kwenda kujenga hospitali katika makao makuu ya nchi Jijini Dodoma.
  • “Huu ndio uwekezaji ninaoutaka, uwekezaji ambao tuna faida nao, Airtel ilikuwepo tangu miaka 8, 9 iliyopita lakini tulikuwa hatupati kitu, sasa tutapata fedha, na hili liwe somo kwetu Watanzania wote kuwa Serikali inapotetea maslahi ya Watanzania haizungumzi kutoka hewani, tujifunze kuwaheshimu watalaamu wetu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
FURAHA YA MAKUBALIANO MUAFAKA:
FURAHA YA MAKUBALIANO MUAFAKA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal na ujumbe wake pamoja na ujumbe wa serikali baada ya kupata picha ya pamoja ya kumbukumbu ya kutiwa saini kwa makubaliano mapya ya ubia kati ya serikali itayokuwa na asilimia 49 na Airteml asilimia 51 kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 15, 2019. Katikati ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi
  • Mhe. Rais Magufuli amemhakikishia Bw. Mittal na wawekezaji wote hapa nchini kuwa Tanzania ni nchi nzuri ya kuwekeza na itadumisha utamaduni wa kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kutambua kuwa uwekezaji huo unasaidia kuzalisha ajira na kuiwezesha Serikali kupata mapato.
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA DAR ES SALAAM ZOO, AVUTIWA NA WANYAMA WENGI WANAOFUGWA HUMO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *