UPASUAJI SARATANI YA MATITI SASA UNAFANYIKA BILA KULIONDOA

  • Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na kampuni ya dawa ya Roche ya nchini Kenya imeandaa mkutano wa kisayansi wa kuwajengea uwezo wataalam wa Radiolojia, Pathiolojia, Upasuaji, tiba ya mionzi na dawa kufanya upasuaji wa saratani ya matiti kwa kutoa uvimbe bila kuondoa titi lote kwa wagonjwa wenye dalili za mwanzoni.

MUHIMBILI

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili -MNH- Prof Lawrence Museru akifungua mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo wataalam wa Radiolojia, Pathiolojia, Upasuaji.

  • Mkutano huo wa kisayansi ambao ni wa kwanza kufanyika katika Hospitali ya Mloganzila umefunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof. Lawrence, umelenga kukumbushana namna bora ya kuwapatia matibabu kwa njia ya kisasa wagonjwa ambao wamethibitika kuwa na saratani ya matiti.
  • Mafunzo hayo yanashirikisha wataalam 30 kutoka Muhimbili pamoja na Hospitali za rufaa nchini ambazo ni Bugando, KCMC, Mbeya na Hospitali binafsi ya Besta.

MUHIMBILI

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila Dkt. Julieth Magandi akiwasilisha mada kuhusu ugonjwa wa saratani ya matiti nchini katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na MNH kwa kushirikiana na kampuni ya dawa ya Roche

Ad
  • Kupitia mtaalam mbobezi kutoka Nairobi, Kenya Dkt. Peter Bird, wataalam hao watapatiwa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa muda wa siku nne ambapo pia mada mbalimbali zinazohusu utoaji wa matibabu ya saratani ya matiti zitawasilishwa.
  • “Nichukue fursa hii kuwashukuru kampuni ya dawa ya Roche kwa kushirikiana na hospitali yetu ili kuwajengea uwezo wataalam hapa nchini kwani wataalam watakaofaidika na mafunzo haya wataenda kuwajengea uwezo wataalam wengine”. Amesema Prof. Museru

MUHIMBILI-MLONAGAZILA

Dkt. Stephen Maina kutoka Roche (wa kwanza kulia) akimkabidhi msaada wa vifaa tiba Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof. Lawrence Museru (Biopsy gun and needle) vitakavyotumika kuchukua sampuli ya uvimbe kwa mgonjwa.

  • Akifafanua amesema saratani ya matiti inachangia vifo kwa wanawake duniani kwa asilimia 25 hadi 35, pia saratani ya matiti ipo kwa kiwango cha juu katika nchi zilizoendelea kuliko nchi zinazoendelea japokuwa vifo vingi vinavyotokana na saratani hiyo hutokea katika nchi zinazoendelea kutokana na wagonjwa kuchelewa kufika hospitalini kwa ajili ya matibabu.
  • Kwa Tanzania saratani ya matiti ni ya pili kwa kusababisha vifo kwa wanawake wenye saratani ikiongozwa na saratani ya shingo ya kizazi, pia katika wanawake 20, mmoja wao yupo kwenye hatari ya kupata saratani hii ya matiti. Vilevile inakadiriwa kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wanaothibitika kuwa na saratani ya matiti nchini Tanzania wanafika hospitalini wakiwa katika hatua ya tatu na ya nne ya ugonjwa ambapo matibabu yake yanakuwa hayatoi matokeo mazuri.
  • Wakati huohuo, Kampuni ya dawa ya Roche imeipatia Hospitali ya Mloganzila msaada wa vifaa tiba (Biopsy gun and needle) vitakavyotumika kuchukua sampuli ya uvimbe kwa mgonjwa.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *