
- Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amesema kuwa wameakabidhiwa rasmi majengo yaliyopo katika Kata ya Changarawe, ambayo yalikuwa yakitumiwa na Mkandarasi wa barabara ya Mafinga – Igawa ili yatumike Kama Kituo cha Afya.
- Mbunge huyo alitoa maombi ya kukabidhiwa majengo hayo kwa Rais Dkt. John Magufuli wakati akitokea katika ziara yake ya Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe mwishoni mwa mwaka 2019


