Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo ameanza ziara ya kikazi kata kwa kata Katika kata mbalimbali za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi.
Akiongea mara baada ya kusikiliza kero za Wananchi Katika kata ya Mbezi juu, Mhe Chongolo Amesema ameamua kushuka chini kwa Wananchi ili kuweza kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi kwani baadhi ya Wananchi wamekuwa hawapati nafasi ya kufika ofisi ya Mkuu wa wilaya kwa lengo la kueleza changamoto zao.
Amesema Katika changamoto 38 alizosikiliza leo, Changamoto nyingi ni za muda mrefu kuanzia miaka 2 Hadi 20, hivyo kwa kuwapatia nafasi ya kuwasikiliza na kuwaunganisha na wataalamu mbalimbali wa Manispaa wanakwenda kutatua migogoro hiyo kwa haraka zaidi.
Nae Diwani wa kata ya Mbezi juu mhe Anna Lukindo amesema wamefurahishwa
na uamuzi wa DC kufika kwenye kata yao na kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili wananchi ikiwemo changamoto za Ardhi, Barabara, Shule na masoko.
Nao Wananchi wa kata ya Mbezi juu hawakusita kutoa shukrani zao kwa Dc kwa kupata fursa ya kumuona na kuweza kutoa changamoto zao ambazo nyingi zimepatiwa ufumbuzi.
Ziara hizi za Dc kutembea Katika kata mbalimbali litakuwa ni utaratibu endelevu kwa kata zote 20 za Manispaa ya Kinondoni ikiwa lengo ni kusogeza huduma ya kuwahidumia Wananchi Katika maeneo Yao.