Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) amewataka Manaibu Makatibu Wakuu wapya, Menejimenti na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza kasi, bidii na ari katika utendaji kazi wa majukumu ili kutoa matokeo yenye tija kwa wananchi.
Katibu Mkuu Nzunda ameyasema hayo leo tarehe 8 Aprili, 2021, Jijini Dodoma, wakati wa kuwapokea Manaibu Makatibu Wakuu wapya wa Ofisi ya Waziri Mkuu walioapishwa Ikulu Jijini Dar Es Salaam, Aprili 6, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Ameeleza kuwa, Ofisi hiyo ina majukumu makubwa ikiwemo kuratibu shughuli za Serikali, hivyo ni muhimu kuongeza nguvu zaidi katika utekelezaji wa majukumu ili kusimamia kwa ufanisi uratibu wa shughuli za serikali.
“Jukumu letu ni kumsaidia Mhe. Waziri Mkuu kutekeleza majukumu ya kusimamia shughuli za serikali, hatunabudi kufanya kazi kwa utaalamu, weledi na kwa kuwajibika kwa kujituma ili kuhakikisha matokea anayo yataka,” alisema Nzunda
Kwa upande wa Manaibu Makatibu Wakuu wapya; Profesa Jamal Adam Katundu na Kaspar Kaspar Mmuya. wameahidi kushirikiana na Watendaji wa Ofisi hiyo kumhakikishia Katibu Mkuu huyo kuwa wapo tayari kufanya kazi kwa kasi ili kupata matokeo chanya kama ilivyo kusudiwa.
Tarehe 6 Aprili, 2021 Ikulu Jijini Dar Es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwaaapisha Manaibu Makatibu Wakuu wa Ofisi hiyo
Michael Jordan https://chicago-bulls.michael-jordan-ar.com is one of the greatest basketball players of all time, whose career with the Chicago Bulls is legendary.
The golf https://arabic.golfclub-ar.com industry in the Arab world is growing rapidly, attracting players from all over the world.