SERIKALI YA TANZANIA NA SEKTA BINAFSI YAFANYA MKUTANO WA KIHISTORIA KATIKA MINING INDABA: KUBORESHA UWEKEZAJI NA KUKUZA SEKTA YA MADINI NCHINI TANZANIA.

Wakati Serikali ya Tanzania na Sekta Binafsi kupitia Chemba ya Migodi Tanzania wakishiriki kwa mara ya kwanza kwa pamoja katika Mkutano wa Mining Indaba nchini Afrika Kusini, wametumia nafasi hiyo kukaa kikao na kujadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuboresha mazingira ya uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania.

Kikao hicho kilichofanyika Februari 4, 2024 katika Hotel ya Hyatt Cape Town, kilihusisha viongozi na wawakilishi wa kampuni kubwa na za kati za uchimbaji wa madini zilizowekeza nchini, pamoja na na watoa huduma migodini, ambapo waliishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya kampuni hizo kwa manufaa ya pande zote mbili.

Ad

 Aidha, kampuni hizo zilitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali kwa kuendelea kufungua milango ya majadiliano ya mara kwa mara na kushauri umuhimu wa kuendelea kutoa nafasi hiyo kwa wadau ikiwemo kutatua changamoto wanazokabiliana nazo katika utekelezaji wa miradi yao.

“Naipongeza Serikali kwa kutoa nafasi hii ya kuzungumza na kutatua changamoto zetu, mfano huu usipoendelezwa, nchi ambazo zinajifunza kutoka kwetu zinaweza kufanya vizuri zaidi yetu ambao tumekuwa mfano mzuri kwa nchi nyingi,’’ alisema Meneja Mkazi wa Kampuni ya Twiga Minerals Melkiory Ngido.

Vilevile, wadau hao walipata fursa ya kutoa maoni na mapendekezo yao ya namna nzuri ya kuendelea kuboresha sekta ya madini nchini. Kwa upande mwingine, kikao hicho kilipata wasaa wa kupitia program za ushiriki wa mzuri wa Tanzania katika mkutano huo.

Kikao hicho kiliwashirikisha Viongozi wakuu wa Wizara wakiongozwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Angelina Mabula, Wakuu wa Taasisi chini ya Wizara ikiwemo Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Kwa upande wa Chemba ya Migodi Tanzania, walioshiriki ni pamoja na Mwenyekiti wa Umoja huo Mhandisi Philbert Rweyemamu, Katibu Mtendaji Mhandisi Benjamin Mchwampaka, Watendaji wa Kampuni za Barrick Gold, Anglo Gold Ashanti, Tembo Nikel, Mamba Minerals, TRX Gold, MANTRA Tanzania, Faru Graphite, City Engineering .

#NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+

Ad

Unaweza kuangalia pia

Benki ya NMB Tanzania yapongezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

kwakuwa Kinara katika utendaji wake, kutengeneza faida kubwa ya mfano wa kuigwa na mashirika na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *