USHAWISHI WA TANZANIA DUNIANI UTATEGEMEA NA UBORA WA SERA YA MAMBO YA NJE INAYOREKEBISHWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu-Zanzibar, Mhe.  Ali Suleiman Ameir akitoa hotuba ya ufunguzi ya Kongamano la Wadau kuhusu kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akitoa neno wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau kuhusu kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024.

Ad

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba kuhutubia Kongamano la Wadau kuhusu kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024.

Watu mbalimbali walioshiriki Kongamano la Wadau kuhusu kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024 

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Justin Kisoka akiwasilisha mada kuhusu maeneo muhimu yanayopendekezwa katika marekebisho ya Sera ya Mambo ya Nje.

Wadau mbalimbali wakifuatilia Kongamano la kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Ikulu Zanzibar, Mhe. Ali Suleiman Ameir amesisitiza umuhimu wa Sera Bora ya Mambo ya Nje inayozingatia maoni ya wadau. Haya yamejiri katika Kongamano la kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania, lililofanyika mjini Zanzibar. Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kushirikisha wananchi katika mchakato huo. Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. January Makamba, ameeleza kuwa Sera ya Mambo ya Nje ni muhimu kwa ushawishi wa Tanzania duniani na marekebisho yanazingatia mabadiliko ya kimataifa. Kongamano limehudhuriwa na viongozi mbalimbali na linajumuisha maoni ya wadau wa ndani na nje ya serikali.

Ad

Unaweza kuangalia pia

“Tusikubali Kuwa Tarumbeta za Watu Wasio Tutakia Mema”

“Tusikubali kuwa tarumbeta za Watu wasio tutakia mema, Maadili Yetu Mazuri Ya Kitanzania Lazima Tuyatunze, …

Oni moja

  1. priligy generic The suspension was stirred 30 minutes and was then filtered through sintered glass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *