WATOTO MILIONI 8 KUPATIWA CHANJO YA SURUA-RUBELLA

1-01
Muuguzi Tumaini Majoji akichanganya dawa wakati wa zoezi hilo
  • Inakadiriwa watoto wapatao 8,028,838 wenye umri wa miezi tisa hadi umri wa chini ya miaka mitano (miezi 59) wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Surua-Rubella kwenye kampeni shirikishi ya chanjo itakayotolewa nchi nzima.
2-01
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na wazazi waliofika kwenye uzinduzi wa chanjo iliyofanyika kwenye viwanja vya jamhuri mkoani morogoro
  • Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoro Ummy Mwalimu wakati akizindua kampeni hiyo iliyofanyika kitaifa mkoani hapa.
4-01
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na mmoja wa mzazi ambaye alipeleka watoto wake mapacha kupatiwa chanjo kwenye uzinduzi huo
  • “Kampeni hii inaanza leo na itamalizika tarehe 21 mwezi huu na itatolewa bila malipo tanzania bara na itaendeshwa katika vituo vya kutolea huduma za afya na vituo maalam vitakavyoundwa na kubainishwa na halmashauri katika kipindi hiki ili kusogeza huduma karibu na walengwa”. Alisema Waziri Ummy Mwalimu.

5-01

  • Aidha, kwa upande wa kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa watoto wenye umri wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na nusu, Waziri huyo alisema inakadiriwa kuwa watoto 4,041,934 watapata chanjo hiyo.
  • “Lengo kuu ni kushiriki katika mkakati wa kitaifa wa kutokomeza ugonjwa wa surua na rubella ili kuchangia katika kupunguza vifo vya watoto hapa nchi,Zoezi hili la kampeni linatarajiwa kugharimu takribani shilingi za kitanzania billion 11.9 sawa na dola za kimarekani milioni 4.59”.
6-01
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) nchini Tanzania Dkt.Tigest Mengestu akizungumza kwenye uzinduzi huo
  • Hata hivyo alisema kuwa chanjo hupunguza gharama kubwa ambazo familia na taifa kwa ujumla lingetumia katika kutibu magonjwa yanayozuilika kwa chanjo“kuna faida kubwa katika uchumi wa taifa tunapowekeza kwenye chanjo,kwani imethibitishwa kwamba kila dola moja unawekeza kwenye chanjo unapata faida ya dola kumi na sita”
7-01
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Lowata Olesanare akiongea na wananchi walofika kiwanjani hapo
  • Naye Mwakili Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tigest Mengestu alisema kuwa Tanzania inatoa chanjo hii kwa asilimia 95 na hivyo kampeni hii inasaidia kuimarisha afya za watoto nchini na kuwakinga na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *