WAFANYABIASHARA, WAWEKEZAJI KUTOKA CZECH WAONYESHA UTAYARI KUWEKEZA TANZANIA

Na Mwandishi wetu, Dar

Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya kilimo hasa Pamba pamoja na viwanda vya nguo hapa nchini.

Ad

Akibainisha kuhusu utayari wa Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Czech, kuwekeza hapa nchini, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek amesema wamefurahishwa sana na mazingira ya biashara hapa Tanzania na wapo tayari kuwekeza katika sekta kilimo na viwanda.

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Dkt. Abdallah Possi akieleza jambo wakati wa mkutano baina ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek na uongozi wa TIC

Staŝek ameyasema hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Kazi leo jijini Dar es Salaam.

Katika ziara yake ya kikazi hapa nchini, Mhe. Staŝek ameambatana na viongozi mbalimbali wa Jamhuri ya Czech akiwemo Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Czech, mhe. Karel Tyll pamoja na Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka nchini humo.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Meh. Miloslav Staŝek amesema yeye pamoja na wajumbe alioongozana nao wamejadiliana na uongozi wa TIC na kupata fursa ya kutambua masuala mbalimbali ya kuongeza ushirikiano ili kuimarisha sekta ya uwekezaji kati ya Czech na Tanzania kwa maslahi ya pande zote mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek akiongea na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Maduhu Kazi leo jijini Dar es Salaam

“Mimi na Timu yangu tumejadili mambo mbalimbali ya kuwekeza hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na utengezaji wa ndege, kilimo, teknolojia pamoja na viwanda.

“Moja ya kampuni niliyoambatana nayo inauzoefu mkubwa katika uzalisha dawa na vifaa tiba, hivyo kampuni hii itakapo pata fursa ya kuwekeza hapa Tanzania itasaidia kuimarisha mahusiano yetu pamoja na kuboresha sekta ya afya,” Amesema mhe. Staŝek.

Mhe. Staŝek ameongeza kuwa wamekubaliana na uongozi wa TIC pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara kutafuta namna bora ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na wale wa Czech ili kutoa fursa kwa kampuni mbalimbali za Czech kuja kuwekeza kwa wingi hapa Tanzania na wafanyabiashara wa Tanzania kuwekeza nchini Czech kwa maslahi ya pande zote mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek akimueleza jambo Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Kazi amesema kuwa mara baada ya mazungumzo ya awali, wawekezaji hao wameonsha nia kubwa sana ya kuwekeza katika Pamba na viwanda vya nguo hapa nchini.

“Wameonesha uwezo mkubwa katika biashara na uwekezaji kwenye maeneo ya ufundi wa ndege ambapo baadae kutakuwa na mafunzo mbalimbali ya kubadilishana ujuzi na fursa za uwekezaji………lakini pia wamevutiwa na sekta ya kilimo hasa katika viwanda vya kutengeneza mafuta ya kula,” Amesema Dkt. Kazi

Mkutano ukiendelea

Nae Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dkt. Abdallah Possi amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa tunatangaza fursa za biashara na uwekezaji.

“Fursa za kupata wafanyabiashara kutoka Zchec zinazidi kuongezeka hapa nchini, hivyo nitoe rai kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa za biashara na uwekezaji,” Amesema Dkt. Posi  

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yaliyolenga kukuza na kuimarisha sekta ya uwekezaji baina ya Tanzania na Czech hapa nchini.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *