Taarifa Vyombo vya Habari

MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA YA SIKU TANO MKOANI SINGIDA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Singida na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi na kupokea taarifa ya mkoa katika ukumbi wa Halmashauri Manyoni. Makamu atakuwa na ziara ya siku 5 mkoani humo.

Soma zaidi »

UJENZI WA RELI YA KISASA DAR ES SALAAM – MOROGORO WAKAMILIKA KWA ASLIMIA 42

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali imedhamiria kwa dhati kukamilisha mradi mkubwa wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), ambapo tayari kiasi cha zaidi ya shilingi trilioni 2 kimetolewa mpaka sasa kwa ajili ya ujenzi huo. Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea …

Soma zaidi »

RAIS MAGUFULI AMETIMIZA NDOTO YA BABA WA TAIFA – MCHENGERWA

Serikali imekabidhi rasmi eneo la mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (RHPP), kwa mkandarasi Kampuni ya Arab Contractors kwa pamoja na ile ya Elsewedy  Electric zote kutoka nchini Misri.  Hatua hiyo sasa inaashiria kuanza kwa kazi ya ujenzi wa mradi huo wa umeme ambao utazalisha Megawati …

Soma zaidi »

MOI WAENDESHA KAMBI YA UPANDIKIZAJI WA NYONGA BANDIA NA UPASUAJI WA MGONGO

Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikianana hospitali ya Zydus ya nchini India kuanzia leo tarehe 14/02/2019 mpaka tarehe 16/02/2019 zitaendesha kambi maalum ya upandikizaji wa nyonga bandia na upasuaji wa Mgongo kwa njia ya kisasa. Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema Katika kambi hii Madaktari bingwa wa …

Soma zaidi »

SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MAZINGIRA WEZESHI KATIKA SEKTA YA KILIMO

Serikali imedhamiria kuendelea kujenga mazingira wezeshi na endelevu katika Sekta ya Kilimo kupitia sera imara na zenye kutekelezeka. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki wakati akifungua Kongamano la Tano la Wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhusu Sera Jijini Dodoma …

Soma zaidi »

KAMPUNI YA JERVOIS YAONESHA NIA KUWEKEZA KABANGA

Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Wawakilishi wa Kampuni ya Jervois Mining Limited ya Australia ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa Nikel- Colbat, Kabanga.  Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko ameendelea kusisitiza kuhusu kufuatwa kwa Sheria na taratibu kwa wenye nia ya kuwekeza katika Sekta ya Madini …

Soma zaidi »

PBPA YATAKIWA KUHAKIKISHA KUWA BANDARI ZOTE ZINATUMIKA KUPOKEA NA KUSHUSHA MAFUTA

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameitaka Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kuhakikisha kuwa bandari zote nchini zinatumika katika shughuli za kupokea na kushusha mafuta ili kuongeza wigo wa upatikanaji  mafuta katika sehemu mbalimbali nchini. Aliyasema  hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake …

Soma zaidi »

MKURABITA INATEKELEZA KWA VITENDO DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2025

Katika  kipindi cha miaka minne (2005 – 2008) uchumi wa Tanzania umeendelea kuimarika na Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7.2 kwa mwaka kuongezeka kutokana na shughuli za kiuchumi katika sekta za viwanda, ujenzi na fedha. Pamoja na mwaka 2009 kuwa ni mwaka ambao kasi ya ukuaji wa …

Soma zaidi »