KAMPUNI YA JERVOIS YAONESHA NIA KUWEKEZA KABANGA

  • Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Wawakilishi wa Kampuni ya Jervois Mining Limited ya Australia ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa Nikel- Colbat, Kabanga.  Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko ameendelea kusisitiza kuhusu kufuatwa kwa Sheria na taratibu kwa wenye nia ya kuwekeza katika Sekta ya Madini na kueleza kuwa, kwa upande wa Wizara, inafanya jitihada za kuondoa urasimu kwenye uwekezaji katika sekta husika.
    WAZIRI WA MADINI
    Waziri wa Madini Doto Biteko (kulia) akimsikiliza mwakilishi wa kampuni ya Jervois Mining Limited ya Australia Balozi Mstaafu Andrew Mcalister (katikati). Kushoto ni Naibu Waziri Stanslaus Nyongo. Wengine ni wawakilishi wa kampuni hiyo.
  • “Tunataka mwekezaji mwenye nia anapoonesha dhamira ya kuwekeza baada ya taratibu zote kukamilika basi aanze mara moja,” amesema Waziri Biteko. Akizungumza katika kikao hicho mmoja wa wawakilishi wa kampuni hiyo Balozi Mstaafu Andrew Mcalister, amesema kuwa, nchi ya Tanzania inaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa madini ya Colbat kutokana na ubora wake na mazingira ya uwekezaji yaliyopo nchini ikiwemo uwazi.
  • Mbali na Waziri Biteko, wengine waliohudhuria kikao hicho ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, na wataalam wengine wa wizara.
Ad

Unaweza kuangalia pia

UCHUMI WA TANZANIA WAZIDI KUKUA NA KUIMARIKA

Hali ya uchumi wa Tanzania yazidi kuimarika na kukua  kwa asilimia 6.9 ikiwa ni  takwimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *