Taarifa Vyombo vya Habari

TANESCO YATENGA TSHS. BILIONI 400 KUPELEKA UMEME KWENYE MAENEO YALIYOPITIWA NA MIUNDOMBINU

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetenga kiasi cha shilingi bilioni 400 kwa ajili ya kazi ya kusambaza umeme kwenye maeneo takribani 754 yaliyopitiwa na miundombinu ya umeme lakini hayana umeme. Hayo yalisemwa tarehe 24 Juni, 2019 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakati wa Majumuisho ya Semina …

Soma zaidi »

MKUTANO WA KUIMARISHA UWEZO WA KIKANDA KWA SEKTA ENDELEVU YA MADINI YA URANI WAFUNGULIWA RASMI

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) wanaendesha mkutano wa siku tano kwa nchi wanachama wa IAEA kanda ya Afrika, zinazodhibiti usalama wa mionzi. Lengo kuu la mkutano huo uliohudhuriwa na jumla ya washiriki 27 kutoka Botswana, Jamhuri ya Afrika …

Soma zaidi »

NAIBU WAZIRI MGALU AWASHA UMEME NJOPEKA MKOANI PWANI

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, jana Juni 23, 2019 alikiwashia rasmi umeme kijiji cha Njopeka kilichopo wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Aliwasha umeme huo kwenye Duka la Abdul Abdulrahman, ikiwa ni ishara ya kukiwashia kijiji kizima. Kabla ya tukio la kuwasha umeme, Naibu Waziri alizungumza na wananchi wa eneo …

Soma zaidi »

SERIKALI KUFANYA UPEMBUZI YAKINUFU KWA AJILI YA UPANUZI WA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE(JKCI)

Tanzania imetia saini Mkataba wa kupatiwa fedha za Msaada wa Shilingi Bilioni 60 za kitanzania kutoka Serikali ya Watu wa China bila ya masharti yeyote ambapo Serikali ya Tanzania itaamua matumizi yake katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wake. Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na …

Soma zaidi »

MAMENEJA TANESCO TUTAWAPIMA KWA KAZI ZENU – NAIBU WAZIRI MGALU

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa wito kwa Mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Ngazi ya Mkoa na Wilaya nchi nzima, kufanya kazi kwa bidii kwani ndicho kigezo kitakachotumiwa kuwapima iwapo wanafaa kuendelea kushikilia nyadhifa hizo. Alitoa wito huo Juni 22, 2019 wakati akizungumza na wananchi wa Mtaa …

Soma zaidi »

DKT. GWAJIMA ATAKA HUDUMA TEMBEZI ZA AFYA KUWA JUKUMU LA PAMOJA

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wadau wote wanaotoa huduma Tembezi za Afya kuunganisha nguvu kwa pamoja ili huduma hiyo iweze kufikishwa katika Halmashauri zote Nchini. Dkt.Gwajima ameyasema hayo wakati wa kikao cha wadau wa Afya kuwasilisha …

Soma zaidi »

MNAPASWA KUDUMISHA NIDHAMU YA MATUMIZI YA FEDHA BAADA YA KUSTAAFU – WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo  Pinda amewaasa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni kudumisha nidhamu katika matumizi ya fedha baada ya kustaafu utumishi wa umma na kujikita katika shughuli za uzalishaji. Akizungumza katika makazi yake yaliyopo Zuzu Jijini Dodoma  wakati …

Soma zaidi »

TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA (TAEC) YAIMARISHA UTENDAJI WAKE KWA KUTUMIA TEHAMA

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imetajwa kuongeza tija katika utendaji wake kutokana na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)katika huduma zake kwa wadau. Akizungumza katika kipindi cha “TUNATEKELEZA”   Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Prof. Lazaro Busagali amesema kuwa Tume hiyo imeimarisha utoaji wa huduma zake kwa …

Soma zaidi »

NAIBU WAZIRI MGALU AZURU KONDOA KUJIRIDHISHA NA ELFU 27 YA UMEME VIJIJINI

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amefanya ziara wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa agizo la Serikali kuhusu kuwezesha wananchi wote wanaopitiwa na miradi ya umeme vijijini (REA), kulipia shilingi 27,000 tu bila kujali ni vijijini au katika Halmashauri za Wilaya. Alifanya ziara hiyo jana, …

Soma zaidi »

TUMEPOKEA MAOMBI MAPYA YA KUUZA MAHINDI TANI MILIONI MOJA KWENDA KENYA – NAIBU WAZIRI MGUMBA

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba amesema Serikali ya Tanzania imepokea maombi mapya ya kuuza mahindi kwenda nchini Kenya yenye jumla ya Tani milioni 1. Mhe. Mgumba ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya gafla kwenye Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA – Makao Makuu) Jijini, …

Soma zaidi »