MKUTANO WA KUIMARISHA UWEZO WA KIKANDA KWA SEKTA ENDELEVU YA MADINI YA URANI WAFUNGULIWA RASMI

  • Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) wanaendesha mkutano wa siku tano kwa nchi wanachama wa IAEA kanda ya Afrika, zinazodhibiti usalama wa mionzi.
  • Lengo kuu la mkutano huo uliohudhuriwa na jumla ya washiriki 27 kutoka Botswana, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Congo, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Misri, Ethiopia, Gabon, Ghana, Madagascar, Malawi, Mali, Nigeria, Sudan na Tanzania ni kujadili na kutoa miongozo kulingana na viwango vya usalama kwa wasimamizi wa nchi za wanachama wa Afrika juu ya utoaji wa leseni na ukaguzi wa shughuli za mzunguko wa uzalishaji wa madini ya urani.
  • Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Injinia John Ben Ngatunga alipokuwa akifungua rasmi mkutano huo katika hotel ya SG Premium Resort ya Jijini Arusha hivi leo, amewataka washiriki wote kufanya majadiliano ambayo yatasaidia kuelewa miundombinu iliyopendekezwa ya sheria na udhibiti wa madini ya urani na majukumu ya washirika wengine wa udhibiti katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

Imetolewa na; Peter G. Ngamilo
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania

Ad

Unaweza kuangalia pia

SOKO LA MDINI ULANGA LA KUSANYA MILIONI 396 NDANI YA MIEZI 5

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema tangu kuanzishwa kwa soko la madini Ulanga wamenunua madini …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *