Taarifa ya Habari

BARAZA LA MAWAZIRI LA RIDHIA KUFUTA DENI LA Sh. BILIONI 22.9 KWA TANESCO KWENYE UMEME ULIOUZWA ZECO

Baraza la Mawaziri limeridhia utozwaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kiwango cha asilimia sifuri kwenye umeme unaouzwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO) na kufuta malimbikizo ya deni la kodi ya VAT lililofikia shilingi Bilioni 22.9 kwa TANESCO kwenye umeme …

Soma zaidi »

TANZANIA KUSHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA YA DUNIA EXPO 2020

Tanzania itashiriki Maonesho ya Dunia ya Biashara (Expo 2020 yatakayofanyika Dubai kuanzia mwezi Oktoba 2020 na kumalizika mwezi April 2021. Uwekaji saini wa Mkataba wa ushiriki wa Tanzania katika Maonesho hayo ulifanywa tarehe 16 Januari 2019 na Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU KUWAPOKEA WATALII 300 KUTOKA CHINA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahidi kupokea kundi la watalii wasiopungua 300 ambao wanatarajiwa kuwasili nchini Machi, mwaka huu. Watalii hao ni kundi la kwanza miongoni mwa watalii 10,000 wanaotarajiwa kuwasili nchini katika mwaka 2019 chini ya mpango unaosimamiwa baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania na …

Soma zaidi »

KIKAO CHA MAWAZIRI KUHUSU BOMBA LA MAFUTA KUFANYIKA KAMPALA WIKI IJAYO

Kikao cha Tatu (3) cha mawaziri wa sekta zinazohusika na utekelezaji wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), kinatarajiwa kufanyika Januari 25, 2019 jijini Kampala. Kikao hicho kitakachotanguliwa na vikao ngazi ya wataalamu na baadaye ngazi ya makatibu wakuu wa Wizara husika, kitaongozwa na Mawaziri …

Soma zaidi »

MRADI WA MADINI YA URANIUM UNATARAJIWA KULIINGIZIA TAIFA KODI YA DOLA MILIONI 220 KWA MWAKA

Uwekezaji uliofanyiwa katika mradi wa uchimbaji madini ya uranium katika mto Mkuju ulioko mkoani Lindi ya Uranium One umefikia kiasi cha dola za kimarekani Milioni mia mbili ($200mil) toka mradi ulipoanza mwaka 2009. Akizungumzia na Waziri wa Madini Dotto Biteko mjini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Uranium One, Frederick Kibodya …

Soma zaidi »

HOSPITAL YA KIBONG’OTO YAJIDHATITI KATIKA UTOAJI TIBA

Hospitali ya Magonjwa ambukizi Kibong’oto inayotoa huduma ya Kifua Kikuu ‘TB’ na magonjwa mengine ya kuambukiza hasa UKIMWI imeendelea kutoa huduma bora kutokana na serikali kuwekeza katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi na tiba. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo Dkt.Riziki Kisonga wakati akizungumza na maofisa …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU APOKEA LESENI YA USAJILI WA TANZANIA SAFARI CHANNEL

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea leseni ya usajili wa chaneli ya utalii ya Tanzania Safari ambayo itaiwezesha kuoneshwa kwa umma bila ya malipo yoyote (a must-carry channel) na wamiliki wa visimbusi. Waziri Mkuu amekabidhiwa leseni hiyo leo mchana (Jumatano, 16 Januari, 2019) kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma …

Soma zaidi »