Taarifa ya Habari

WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KOROMIJE

Waizri Mkuu Kassim Majaliwa amefungua mradi wa ujenzi na ukarabati mkubwa wa kituo cha afya cha kata ya Koromije wilayani Misungwi na amewahakikishia wananchi kuwa Serikali imejipanga vizuri kuboresha huduma za afya. Amesema uboreshaji huo unahusisha ujenzi wa chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, wodi ya mama na mtoto …

Soma zaidi »

VIJANA WAANZA KUITIKIA WITO WA KUCHAPA KAZI KIZALENDO

Vijana wa kijiji cha Chihwindi kata ya Mtumachi, Newala mkoani Mtwara wamefyeka uwanja  wa kijiji hicho kwaajili ya ujenzi wa kiwanja hicho cha timu ya kijiji maarufu kwa jina la POCHI NENE. Akizungumzia tukio hilo Ndugu Musa Shaibu, amesema kuwa wamefanya hivyo kwa lengo la kuhamasisha vijana kujitolea kufanya kazi …

Soma zaidi »

SERIKALI INATEKELEZA UJENZI WA MITAMBO 55 YA BIOGAS

Miradi ya Viwanda: Kiwanda cha Kuunganisha Matrekta (TAMCO, Kibaha): Hatua iliyofikiwa ni: kuingiza matrekta 822 aina ya URSUS (semi knocked down) ambapo matrekta 571 yameunganishwa na matrekta 339 yameuzwa; Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini – CAMARTEC: kutengeneza zana zikijumuisha mashine 64 za kupandia mbegu za pamba, kusaga …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA SOKO LA DHAHABU MJINI GEITA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa tahadhari kwa wadau wote wa madini kuwa atakayekamatwa anatorosha madini, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo utaifishaji wa madini atakayokuwa akiyatorosha. Pia amewataka viongozi na watendaji wote wa Serikali wasimamie kwa weledi, uaminifu na uadilifu, sheria, kanuni na miongozo kuhusu sekta ya madini kwa lengo la …

Soma zaidi »

SERIKALI INAPENDA KUWAHAKIKISHIA KUWA CHANGAMOTO ZA WALEMAVU ZINAFANYIWA KAZI – MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahimiza watu wenye ulemavu kutumia fursa zilizopo katika kujikwamua kiuchumi. Makamu wa Rais ameyasema hayo  kwenye hafla ya utoaji tuzo ya I CAN kwa watu wenye ulemavu iliyoandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Foundation, iliyofanyika leo …

Soma zaidi »

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA RELI YA KISASA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), unaoanzia Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa KM 300 na  kusisitiza kuwa Bunge litaendelea kupitisha fedha za mradi huo hadi utakapokamilika kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Mwenyekiti wa Kamati …

Soma zaidi »

ZANZIBAR KUTOA USHIRIKIANO KWA SHIRIKA LA NGUVU ZA ATOMIKI DUNIANI

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Simai Mohamed Said amesema Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano kwa shirika la nguvu za atomiki Dunia  ili kukuza na kuimarisha teknolojia ya utumiaji wa mionzi. Ameyasema hayo katika mkutano wa pamoja na ujumbe wa shirika la Nguvu za Atomic Duniani (IAEA) kanda …

Soma zaidi »