VIJANA WAANZA KUITIKIA WITO WA KUCHAPA KAZI KIZALENDO

VIJANA
Vijana wa kijiji cha Chihwindi wakifyeka uwanja kwa ajili ya michezo 
  • Vijana wa kijiji cha Chihwindi kata ya Mtumachi, Newala mkoani Mtwara wamefyeka uwanja  wa kijiji hicho kwaajili ya ujenzi wa kiwanja hicho cha timu ya kijiji maarufu kwa jina la POCHI NENE.
  • Akizungumzia tukio hilo Ndugu Musa Shaibu, amesema kuwa wamefanya hivyo kwa lengo la kuhamasisha vijana kujitolea kufanya kazi ambazo zipo ndani ya uwezo wao badala ya kusubiri kufanyiwa kazi  na Serikali
VIJANA
kazi ikiendelea ya kufyeka kiwanja hicho
  • “Tumeamua kufanya  kazi hii ya kufyeka uwanja huu ili kuisadia timu ya kijiji chetu kupata uwanja wa kufanyia mazoezi kwa lengo la kukuza michezo kwani kuna vijana wengi wenye uwezo mkubwa katika michezo lakini wanakosa sehemu za kufanyia mazoezi”amesema Musa
  • Aidha amesema kuwa watafanya harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya kununua vifaa mbali mbali vya michezo vinavyohitajika kwa ajili ya timu ya kijiji hicho,ameongeza kuwa wameafanya hivyo ili vijana wajipatie ajira kupitia michezo kwani michezo ni moja ya sekta ambayo inatoa ajira kwa vijana.
Ad

Unaweza kuangalia pia

MATUKIO YA WAZIRI MKUU BUNGENI MJINI DODOMA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *