TUSIMAMIE WAKANDARASI WANAOJENGA MJI WA SERIKALI DODOMA

  • Manaibu Mawaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua kiwanja kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara hiyo ambapo Serikali imetoa shilingi bilioni moja kwa kila Wizara na kuelekeza kuwa ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu Wizara zote ziwe zina majengo yake ya ofisi kwenye mji wa Serikali uliopo Ihumwa mkoani Dodoma
  • Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akiambatana na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa na Katibu Mkuu wa Mawasiliano Mhandisi Dkt. Maria Sasabo na wataalamu wa Wizara hiyo wametembelea na kukagua eneo lenye ukubwa wa ekari 6.3 ambalo limetengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano lililopo Ihumwa mkoani Dodoma ambalo litagharimu jumla ya shilingi bilioni 1.120 na litajengwa na Vikosi vya Ujenzi, tawi la Dar es Salaam
  • Kwandikwa amesema kuwa Serikali imetupa dhamana kubwa ya kuwa wakandarasi na kusimamia majengo ya Wizara zote, sisi kama Wizara tujenge vizuri kweli kweli ili tuwe mfano wa kuigwa na Wizara nyingine na tusimamie wakandarasi wengine wa JKT, NHC ambao wamepewa jukumu la kujenga ofisi za Wizara nyingine kwa kuwa sisi ndio wenye dhamana ya kusimamia wakandarasi wote nchini kama lilivyo agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa kassimu Majaliwa.
  • Ameongeza kuwa tuko tayari kukesha na kukesha ili kuhakikisha kuwa tunafanya kazi usiku na mchana DODOMA-1
  • Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiiano Mhandisi Atashasta Nditiye ameiomba Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dodoma iweze kufikisha maji ya kutosha kwenye eneo hilo kwa ajili ya kufanikisha shughuli za ujenzi ii ziweze kukamilika kwa wakati uliopangwa na Serikali ili waweze kuendelea kuwahudumia wananchi.
  • Pia, ameongeza kuwa taasisi zinazohusika na masuala ya mazingira nazo ziangalie namna ya kufanikisha upandaji miti kwenye eneo la mji wa Serikali ili kuweka mazingira mazuri kwenye maofisi yanayojengwa kwenye mji huo.
  • Aidha, amewashukuru TANESCO kwa kufika eneo husika na kuanza kujenga nguzo kwa ajili ya kusambaza umeme, “ni imani yetu kuwa ujenzi utaisha tarehe 30 Desemba mwaka huu ili tuweze kuingia tarehe 31 Desemba mwaka huu,” amesema Nditiye.
  • Naye Katibu Mkuu wa Mawasiliano Mhandisi Dkt. Maria Sasabo wakati akiwaonesha Nditiye na Kwandikwa eneo hilo la ujenzi alisema kuwa ofisi hizo zitatumika kwa ajili ya Waziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Katibu Mkuu na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo ili kuweza kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kuhakikisha kuwa Wizara zote zinaendesha shughuli zake kwenye mji wa Serikali, Ihumwa.
DODOMA-2
  • Naye Mkurugenzi wa Barabara, Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Happiness Mgalula akimwakilisha Katibu Mkuu wa Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamuhanga amesema kuwa tayari michoro imekamilika na makubaliano ya ujenzi wa ofisi hiyo yamefanyika ambapo mkataba utasainiwa leo baina ya Wizara na Vikosi vya Ujenzi, tawi la Dar es Salaam ili waaanze kazi hiyo mara moja
  • Mkurugenzi Msaidizi Majengo ya Serikali, Sekta ya Ujenzi, Msanifu Majengo Edwin Nnduma amesema kuwa makadirio ya ujenzi huo hapo awali yalikuwa shilingi milioni 983,437,600 ambapo kuendana na uwepo wa idadi ya viongozi wa Wizara na ongezeko la mahitaji ya ukumbi wa mikutano, Wizara imelazimika kuongeza fedha kiasi cha shilingi milioni 160 ili kuhakisha kuwa ujenzi unaendana na mahitaji ya ofisi.
Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.