UKARABATI WA KIVUKO CHA MV. PANGANI II WAKAMILIKA

1-01
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto, Mhandisi Mahangaiko Ngoroma na Mkuu wa kivuko cha Pangani Mhandisi Abdulrahman Ameir wakishuka kutoka kivuko cha MV. PANGANI II. Kivuko hicho kimefanyiwa ukarabati mkubwa ikiwemo kubadilishiwa mfumo mpya wa kuweza kufanya kazi kwenye maji ya bahari (maji chumvi) tofauti na awali ambapo kilikuwa kikifanya kazi kwenye maji ya Mto (maji baridi), awali kilikuwa kikitoa huduma kati ya Utete na Mkongo Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kikijulikana kama MV. UTETE ambapo kilishindwa kuendelea kutoa huduma maeneo hayo kutokana na changamoto ya kupungua kwa kina cha maji kwa muda mrefu katika Mto Rufiji. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50. PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA TANGA)
2-01
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akiingia kukagua chumba cha kuongozea kivuko cha MV. PANGANI II. Kivuko hicho kimefanyiwa ukarabati mkubwa ikiwemo kubadilishiwa mfumo mpya wa kuweza kufanya kazi kwenye maji ya bahari (maji chumvi) tofauti na awali ambapo kilikuwa kikifanya kazi kwenye maji ya Mto (maji baridi), awali kilikuwa kikitoa huduma kati ya Utete na Mkongo Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kikijulikana kama MV. UTETE ambapo kilishindwa kuendelea kutoa huduma maeneo hayo kutokana na changamoto ya kupungua kwa kina cha maji kwa muda mrefu katika Mto Rufiji. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI KUPELEKA MAWASILIANO YA SIMU SINGIDA MASHARIKI

Serikali imeahidi kujenga mnara wa simu katika Kijiji cha Msule kilichopo kata ya Misugha jimbo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *