TANZANIA KINARA WA KUVUTIA WAWEKEZAJI AFRIKA MASHARAIKI

  • Tanzania imeendela kuweka rekodi ya kuvutia wawekezaji kwa nchi zilizopo ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwa na mtaji wa uwekezaji wa Dola Bilioni 1.18, ikifuatiwa na Uganda wenye uwekezaji wa dola za kimarekani 700
  • Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Godffrey Mwambe amesema nchi ya Kenya inashika nafasi ya Tatu wakiwa na uwekezaji wa dola za kimarekani 670 na hivyo kuiweka Tanzania kuwa juu ya nchini zingine Afrika Mashariki.
  • Mwambe amesema kuwa Tanzania inaongoza kuvutia wawekezaji kutokana na mapinduzi makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ambapo hadi sasa imewekeza jumla ya miradi mipya 905 katika sekta mbalimbali nchini miradi ambayo itatengeneza ajira 115,055 kwa watanzania na kuleta tija na manufaa kwa taifa
  • Alisema kuwa katika kipindi hiki cha miaka mitatu TIC imeweza kuvutia wawekezaji na kuweza kuandikisha, mfano kuanzishwa kwa viwanda mbalimbali ambavyo vimeweza kuongeza pato la Taifa.
  • Akifafanua zaidi anasema kuwa baadhi ya miradi mikubwa zaidi iliyowekezwa nchini ni pamoja na ikiwemo kiwanda cha Goodwill Ceremics Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani kinachojihusisha na utegenezaji vigae na kimewekeza jumla ya dola za kimarekani milioni 53, huku kikitoa ajira za moja kwa moja 1500 kwa watanzania na ajira zisizo za moja kwa moja 3,000.
  • “Viwanda vingine ambavyo vimeiwezesha Tanzania kuwa kinara wa kuvutia wawekezaji ni KEDA (Twyford) Tanzania ceramic Ltd pia ni cha kutengeneza marumaru na hiki ni kikubwa zaidi kina mtaji wa Dola za kimarekani milioni 56, kimetoa ajira za moja kwa moja zipatazo 2,000 kwa watanzania na ajira zisizo za moja kwa moja 4,000” alisema.
  • Anavitaja Viwanda vingine kuwa ni Sayona Friut Ltd yenye mtaji wa milioni 55, KEDS(T) Co.Limited mtaji wa dola milioni 11.8 pamoja na kiwanda cha nondo cha Kiluwa Steel Group ambacho ni kikubwa kwa ukanda wa afrika mashariki kina mtaji wa dola milioni 130 na kinazalisha jumla ya tani 200 za nondo.
  • Aidha Mwambe alieeleza nchi zinazoongoza kwa kuwekeza nchini Tanzania ni pamoja na Jamhuri ya Watu wa China, Uingereza na Marekani.
  • “Maendeleo ya China yaliyopatikana kwa miaka 40 kwa watanzania wote ni funzo kubwa la kuwa na uzalendo, China ndiyo inaongoza kuwa kuwekeza nchini tangu miaka ya 1990, na kwa sasa ina miradi ya uwekezaji 723”, Mwambe Mkurugenzi Mkuu, TIC.
  • Alibainisha utaoji huduma, Mwambe anasema TIC imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika utoaji huduma kwa wateja ndani na nje ya nchi kwani kwa sasa huduma zote zinazomuhusu mwekezaji zinapatika TIC kupitia mfumo wa ‘Huduma za mahala pamoja’ ambapo huduma hii imeongeza wawekezaji kwa kuvutiwa zaidi na kuwezesha Tanzania kuwa kinara katika nchni za Afrika Mashariki.
  • “Tumefanikiwa kuongeza Taasisi ambazo hazikuwepo katika huduma za mahala pamoja ndiyo maana tuliwatafuta kwenye maofisi yao na kuwaleta hapo katika Taasisi kama NIDA, OSHA,NEMC, TBS, TFDA pamoja na TANESCO , hawa wamekuja kuimarisha na kuondoa usumbufu kwa wawekezaji na sasa tunaongelea jambo la kuwa kinara wa kuvutia wawekezaji Afrika Mashariki” Mwambe.(Paschal Dotto-MAELEZO)
Ad

Unaweza kuangalia pia

KILA MTANZANIA ANAWEZA KUWEKEZA, TUMIENI FURSA ZILIZOPO – WAZIRI KAIRUKI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *