Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikabidhiwa nyaraka mbalimbali na Mkurugenzi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Bi. Haigath Kitala mara baada ya mkurugenzi huyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wakati wa ziara ya kikazi ya Dkt. Mwanjelwa katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam, ziara ilikuwa na lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji.

MFUKO WA RAIS WA KUJITEGEMEA(PTF) UNAFANYA VIZURI – NAIBU WAZIRI MWANJELWA

 • Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) umepongezwa kwa utekelezaji mzuri wa Sera ya Uchumi wa Viwanda inayohimizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa mikopo kwa makundi maalumu ya watu wenye ulemavu, akina mama na vijana wanaojihusisha na shughuli za ujasiriamali jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwasisitiza watumishi wa PTF kutoa huduma nzuri kwa walengwa wa mikopo inayotolewa na PTF wakati wa ziara ya kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.
 • Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kuwatembelea watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea  kwa lengo la kufahamu majukumu ya mfuko huo na kuhimiza uwajibikaji, ambapo alipata fursa ya kujionea wanufaika wa mikopo inayotolewa na mfuko huo.
 • Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, makundi yaliyopatiwa mikopo ambayo ni kundi maalumu la walemavu la Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi Tanzania (FUWAVITA), kikundi cha UWAZI  SHALOOM cha akina mama wasindikaji, Kikundi cha MAKINI FOOD SUPPLIES cha akina mama wasindikaji na kikundi cha MAB cha vijana ni mfano mzuri wa kuigwa kwa kutekeleza sera ya Uchumi wa viwanda kwa vitendo kwani wanazalisha bidhaa zenye ubora ambazo ni mvinyo, viungo vya mchuzi, viungo vya chai, siagi ya karanga, mango pickle na mabeji ya wanafunzi wa shule za awali, za msingi na vyuo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi Tanzania (FUWAVITA), kikundi cha UWAZI SHALOOM cha akina mama wasindikaji, Kikundi cha MAKINI FOOD SUPPLIES cha akina mama wasindikaji na kikundi cha MAB cha vijana wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.
 • Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, PTF imejitofautisha na taasisi nyingine za kifedha kwani  inajali makundi maalumu yote kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu na yenye riba ndogo zaidi bila ubaguzi wowote.
 • Kwa upande wake, mwakilishi wa kikundi cha Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi  Tanzania (FUWAVITA), Bi. Aneth Gerana amesema wanaishukuru PTF kwa kuwapatia mikopo kwani imekuwa ikiwanufaisha sana ikizingatiwa kwenye mabenki hawadhaminiki hivyo PTF imekuwa mkombozi kwao.
 • Bi. Gerana amesisitiza kuwa, kupitia mkopo wa fedha wa PTF wao kama walemavu wameweza kuuthibitishia umma kuwa, wanaweza kwa kuzalisha mvinyo wenye ubora na kuongeza kuwa wana hakika ya kuifikia ndoto ya kuwa na kiwanda cha mvinyo kikubwa Afrika ya Mashariki ili kuunga mkono kwa vitendo sera ya uchumi wa viwanda ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) wakati wa ziara ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji, ambapo pia alipata fursa ya kujionea wanufaika wa mikopo inayotolewa na mfuko huo.
 • Bi. Gerana, ameiomba PTF kuwapatia mafunzo ya kompyuta wao kama kundi maalumu la walemavu ili mafunzo hayo yaweze kuwasaidia kutafuta masoko kwa njia ya mtandao,  ombi ambalo lilitiliwa mkazo na Mhe. Dkt. Mwanjelwa kwa kuitaka PTF kuwapatia mikopo ya vifaa itakayowawezesha kununua kompyuta zitakazowarahisishia  utafutaji wa masoko kwa njia ya mtandao.
 • Naye, Mwakilishi wa kikundi cha MAB cha vijana wanaotengeneza mabegi, Bw. Amon Philemon amesema mkopo wa PTF umewawezesha kuwa wajasiriamali wa  kutengeneza mabegi ya wanafunzi wa kuanzia shule za awali hadi vyuo vya elimu ya juu.
 • Bw. Philemon ameainisha kuwa, katika mabegi wanayoyatengeneza wanaweka picha za wanafunzi husika, majina yao na logo,  lengo likiwa ni  kudhibiti wizi mashuleni na vyuoni, hivyo Dkt. Mwanjelwa amekipongeza kikundi hicho kwa ubunifu huo.
 • Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) ni Taasisi ya Kifedha inayotoa mikopo ya fedha na vifaa nchini kwa makundi ya akina mama wajasiriamali wazalishaji, kundi maalumu la watu wenye ulemavu na vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi stadi, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi lengwa kabla ya kutoa mikopo kwa wanufaika hao wa PTF.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

2 Maoni

 1. KAGANDA elizabeth

  Mfuko was rais mkoa wamorogoro ulitukomboa sn sisi akina mama wajane ,tangu nilipojiunga nilipata mafanikio makubwa nawazo yaliisha kwani niliamini nipo kwenye chombo salama,lkn walipokuja akina dastani wakatuvuluga mkasitisha uduma,baadae uduma zikaanza Tena kwa ishawishi mkubwa tukajiunga Tena,Sasa chakusikitisha nikwamba toka tr 23-1-2019,tumemaliza mikopo Lkn hakuna uduma Tena,akina zetu hatupewi tukipiga sima tukauliza tunaambiwa tatizo liko makao makuu,Sasa ndio uduma Bora tunazopata kweli maana ata uzalishaji uyoga tumesidha mashamba yamekufa,hatujui hatma zetu,bc tupewe viakiba vyetu tujue Nini tufanye,mh mwenye dhama na kilio iki kikufikie najua unatujali akina mama wenzio,tunaangamia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *