JAJI MSTAAFU MARK BOMANI AWATAKA WATANZANIA KUCHANGIA FURSA KATIKA SEKTA YA MADINI

  • Mwanasheria mkuu wa kwanza Tanzania Jaji Mstaafu Mark Bomani amewataka watanzania kuchangamkia fursa ya mabadiliko ya sheria katika sekta za maliasili na madini yaliyofanyika hivi karibuni,kutokana na sheria hizo kuweka mazingira ya usawa (win – win situation)tofauti na sheria zilizokuwepo awali kutoa kipaumbele kwa wawekezaji kutoka Nje ya nchi.
  • Jaji Mstaafu Mark Bomani ameyasema hayo alipomtembelea ofisini kwake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu sekta ya madini nchini na kuongeza kuwa Tanzania ina utajiri mkubwa wa madini unaotosha kuendesha Nchi  ukiachilia mbali maliasili nyingine zilizopo tatizo ni kuwa madini hayo hayakulinufaisha Taifa.
  • Mabadiliko ya sheria waliyoyafanya yatasaidia sana,sasa ni jukumu letu sisi Watanzania kuichangamkia fursa hiyo na tusisubiri kulalamika kama ilivyo kawaida yetu,tfanye kazi kwa bidii maana utajiri huu wa madini tuutumie na kujiletea maendeleo binafsi na yanchi kwa ujumla kwa kuwa sasa sheria hizi mpya zimeweka uwanja sawa”
WAZIRI KABUDI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (kushoto) akiwa na mgeni wake Jaji Mstaafu Mark Bomani alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam.
  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi mbali na kumshukuru Jaji Mstaafu Mark Bomani kumtembelea ofisini kwake ameongeza kuwa mabadiliko yaliyofanyika katika sheria za madini yametokana kwa kiasi kikubwa na ripoti ya tume iliyoundwa kuchunguza sekta ya madini ikiongozwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani.
  • “Haya yoote tuliyoyabaini na kuyaeleza kama upungufu yamo kwenye ripoti ya Bomani ingawa kuna mengine tuliyoyaongeza kama vile mrahaba ulio chini,kutolipa kodi na mengine mengi na kwakuwa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameutangaza mwaka 2019 kuwa mwaka wa uwekezaji,Mzee Bomani amekuja ili tubadilishane mawazo tuone namna ya kuuboresha mwaka huu wa uwekezaji”
  • Ameongeza kuwa wamezungumzia namna ya kuweka mikakati ya kuwavutia wawekezaji wenye tija kuja nchini kuwekeza ili Taifa liweze kunufaika na madini kupitia kodi,ajira kwa vijana na kwamba ujio wa Jaji Mstaafu Mark Bomani ofisini kwake umemjengea ari na nia ya kuonana na viongozi wengine waliolitumikia Taifa kwa tija ili aweze kupata maoni yao ya namna ya kuendesha shughuli za serikali katika wizara aliyopangiwa kazi na Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI ZUNGU AHUDHURIA MKUTANO WA 7 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA MAZINGIRA NA MALIASILI WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI

             

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *