Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akiongea Jambo na Mawaziri wengine waliohudhuria Mkutano wa saba wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Maliasili wa Jumuia ya Afrika Mashariki uliofanyika Dodoma. Mawaziri wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii- Mhe. Hamis Kigwangala, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya nje na Usirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Damas Ndumbaro na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu pamoja na Mawaziri wengine waliohudhuria Mkutano wa saba wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Maliasili wa Jumuia ya Afrika Mashariki uliofanyika Dodoma wakiimba wimbo maalum wa Jumuia ya Afrika Mashariki.Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano huo wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Maliasili wa Jumuia ya Afrika Mashariki uliofanyika Dodoma wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokua ikitolewa wakati wa Mkutano huo.