BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeidhinisha jumla ya Shilingi bilioni 55,175,163,302 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo kwa Wizara ya Katiba na Taasisi zake.
  • Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 47,283,566,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na mishahara na shilingi Bilioni 7,891,598,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
  • Fedha zilizopitishwa ni kwa ajii ya Ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria, Tume ya Utumishi wa Mahakama,Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Tume ya Kurekebisha Sheria.
  • Wizara pia iliomba Bunge liidhinishe shilingi Bilioni 126,162,464,756 kwa ajili ya Mfuko wa Mahakama . Kati ya Fedha hizo shilingi Bilioni 104,004,564,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi Bilioni 22,157,900,576 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI MKUU AMPONGEZA BONDIA SALIM MTANGO ALIYESHINDA MKANDA WA DUNIA WA UBO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *