Jengo la Utawala

MAENDELEO YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA UYUI, KUMALIZIKA MWEZI JUNI

STOO YA DAWA
Jengo la stoo ya Dawa katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora lilipofikia.
  • Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Uyui unatarajia kukamilika mwishoni mwa Mwezi ujao tayari kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
  • Kauli hiyo imetolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati akielezea maendeleo ya ujenzi wa majengo saba ya Hospitali hiyo.
OPD
Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora lilipofikia.
  • Alisema kwa upande wa jengo la Utawala tayari yameezekwa na kuwekewe miundo ya umeme na maji na kwa jengo la kufulia limeshaezekwa.
  • Msuya alisema kwenye jengo la wagonjwa wa nje(OPD) , jengo la uchunguzi wa mionzi, na , maabara iko kwenye lenta na jengo la stoo ya dawa liko katika hatua ya upauaji baada ya kumaliza hatua ya kufunga lenta.
MIYONZI
Jengo la huduma ya uchunguzi wa mionzi katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora lilipofikia.
  • Alisema kwa upande wa jengo la mama na mtoto liko katika hatua ya kuanza kufungwa lenta.
  • Mkuu huyo wa Wilaya alisema wanatarajia kumaliza ujenzi katika kipindi kilichopangwa.
  • Kaimu Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora Akwilin Mwachali alisema hivi wanakwenda kwa kasi baada ya kuvunja mkataba na baadhi ya mafundi wa awali na kukabidhi shughuli kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
MAMA NA MTOTO
Jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora lilipofikia.
  • Alisema mafundi wa awali walikuwa wakifanyakazi pole pole na wakati mwingine wakishindwa kufika kazini kwa visingizio mbalimbali na ndio waliona wachukue hatua ya kusitisha mkataba ili waweze kumaliza kazi hiyo kwa wakati.
  • Mkazi wa Ilalansimba wilayani Uyui John Kulwa ameishukuru serikali kwa kuwajengea Hospitali ya Wilaya kwa kuwa imesaidia kutokwenda mbali kufuata huduma za ngazi ya Hospitali ya Wilaya.
MAABARA
Jengo la uchunguzi wa maabara katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora lilipofikia.
KUFULIA
Jengo la kufulia katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora lilipofikia. NA TIGANYA VINCENT
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *