MKUTANO WA TUME YA USHIRIKIANO WA TANZANIA NA UGANDA WAANZA DAR ES SALAAM

 

  • Mkutano wa tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, umeanza leo Septemba 3, 2019 jijini Dar es Salaam.
  • Mkutano huo wa siku tatu pamoja na mambo mengine, unatarajiwa kupokea taarifa ya Wizara ya Nishati ya Tanzania kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya Mkutano wa Pili wa Tume husika, uliofanyika Agosti, mwaka jana.
  • Taarifa hiyo ya Wizara imejikita katika masuala ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika bonde la Eyasi Wembere, bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania (EACOP) na ujenzi wa bomba la kupeleka gesi asilia nchini Uganda.
  • Mingine ni miradi ya umeme ikiwemo mradi wa umeme wa maji wa Nsongezi, njia ya kusafirisha umeme ya Masaka – Mtukula – Mwanza pamoja na miradi mingine ya umeme inayotekelezwa mpakani mwa nchi husika.
  • Sekta nyingine zinazohusika katika Mkutano huo ni pamoja na Ulinzi na Usalama; Maendeleo ya Miundombinu na Usafirishaji; Viwanda, Biashara na Uwekezaji; Utalii; Kilimo, Uvuvi na Mifugo; Maji na Mazingira; Afya; Elimu na Mafunzo; Habari pamoja na sekta ya Utamaduni.
  • Katika siku ya kwanza ya Mkutano ambayo ni leo, wahusika ni wataalamu kutoka pande zote mbili; ambao utafuatiwa na ngazi ya Makatibu Wakuu kesho Septemba 4, kisha kuhitimishwa kwa ngazi ya Mawaziri, Septemba 5, 2019.Na Veronica Simba – Dar es Salaam
Ad

Unaweza kuangalia pia

TPDC YAOKOA TRILIONI 12.7 KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *