WAZIRI KALEMANI AFUNGUA KIWANDA CHA NGUZO ZA UMEME – KIGOMA

7-01
Waziri wa Nishati, Dkt Kalemani akimpongeza Leonard Mahenda ambae ndio mmiliki wa kiwanda cha Qwihaya mara baada ya kukata utepe.
  • Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amefungua kiwanda cha Nguzo cha Qwihaya, kilichopo katika Mtaa wa Kasanga, Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma
  • Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara, mara baada ya ufunguzi wa kiwanda hicho Dkt. Kalemani alieleza kuwa Serikali ilikuwa inapata gharama kubwa kutoa Nguzo katika Mikoa mengine kuzifikisha Mkoani humo kabla ya kiwanda hicho kujengwa Mkoani humo.
8-01
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani( wa kwanza kulia), Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga wakiwa kwenye ufunguzi wa kiwanda cha Nguzo za Umeme cha Qwihaya.
  • Alisema, maeneo ambayo yapo karibu na kiwanda hicho yatafikiwa na umeme kwa haraka kwasababu hakutakuwa na sababu ya ucheleweshaji wa kupeleka umeme katika maeneo hayo ambayo, kiwanda cha nguzo kipo karibu.
  • Aliongeza kuwa, Serikali haitakubali kuona ucheleweshwaji wa usambazaji umeme vijijini, kupitia TANESCO au Wakandarasi, kwasababu ya uwepo wa kiwanda hicho Mkoani humo umewarahisishia kazi na bei ya nguzo itashuka ikilinganishwa na bei ya Nguzo ambazo zinatoka katika Mikoa ya Njombe na Iringa.
6-01
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kiwanda cha nguzo cha Qwihaya.
  • “ Maelekezo yangu kwa TANESCO ni kuanza kuzichukua nguzo hizi kwa njia ya ushindani hakuna tena sababu ya kusema nguzo hakuna na nataka kazi zimalizike ndani ya muda kwasabau vitendea kazi vipo na pesa ipo” alisema.
  • Alifafanua kuwa, mahitaji ya nguzo kwa sasa nchini ni milioni moja na nusu kwa mwaka lakini wazalishaji nchini wanauwezo wa kuzalisha zaidi ya nguzo milioni tatu ukilinganisha na mwaka 2015 ambapo mahitaji ya nguzo yalikuwa milioni moja na nusu lakini nguzo zilizokuwa zinapatikana nchini ni laki nne tu, ambapo nguzo nyingi zilikuwa zinatoka Nchi za nje lakini kwa uwepo wa viwanda nchini imesaidia sana upatikanaji wa nguzo kwa wingi.

5-01
Mmoja wa mtambo inayotumika kuzalishia nguzo za umeme katika kiwanda cha Qwihaya kilichopo wilayani Kasulu.
  • Alieleza kuwa, kwa kipindi cha miaka minne viwanda vya nguzo tisa vimejengwa nchini, mara baada ya Serikali kupiga marufuku ya ununuaji nguzo kutoka nchi za nje ambao ulikuwa unachelewesha usambazaji wa umeme nchini .
  • Aidha, alimpongeza muwekezaji wa kiwanda hicho, kwa kujitolea kujenga kiwanda kwenye eneo hilo pamoja na kumiliki viwanda vyengine Mkoani Njombe na Iringa na kuamua kuwekeza katika maeneo mengine ya nchini.
3-01
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( mwenye shati la bluu) akiwasili kwenye ufunguzi wa kiwanda cha Nguzo cha Qwihaya kilichopo wilayani Kasulu.
  • Kwa kuona umuhimu wa Viwanda hivyo, Waziri Kalemani ametoa wito kwa wawekezaji wengine wajitokeze kujenga viwanda vya Nguzo, katika Mikoa mengine nje ya Mkoa wa Iringa na Njombe ili kutimiza azma ya Rais ya Tanzania ya Viwanda.
  • Awali, Kaimu Mkurugenzi wa kiwanda hicho Beruto Kaboda ameleza kuwa kiwanda chao kimeamua kimeitikia wito wa Rais, wa Tanzania ya Viwanda kwa vitendo kwa kuchukua hatua ya kujenga kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya nguzo laki moja kwa mwaka.
2-01
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, akipata maelekezo kuhusu kiwanda cha Qwihaya kutoka kwa mmoja wa mfanyakazi wa kiwanda hicho.
  • Vile vile, alieleza kuwa kwasasa soko lao kubwa lipo hapa nchini na mteja wako mkubwa ni Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) ambapo kipindi hiki cha utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu soko la nguzo limekuwa kubwa na kuwalazimu kufanya kazi kwa masaa 24.
  • Pia alitoa shukrani zake kwa Waziri wa Nishati Dr Medard Kalemani na Naibu Waziri Subira Mgalu kwa kuwasimamia wazalishaji wa nguzo nchini na kutoa miongozo ambayo inawapa hamasa ya kufanya kwa bidii na kuhakikisha wanazalisha nguzo bora na zinawafikia wananchi wa vijiji kwa haraka zaidi.
  • Hafsa Omar-Kigoma
Ad

Unaweza kuangalia pia

UUNGANISHAJI UMEME VIJIJINI UENDE SAMBAMBA NA IDADI KUBWA YA KUWAWASHIA WATEJA

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amewaagiza Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini(REA) pamoja …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *