WAZIRI KALEMANI AKUTANA NA WAZALISHAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI

  • Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, amekutana na wazalishaji binafsi wa umeme nchini na kujadiliana masuala mbalimbali ya kuboresha zaidi sekta hiyo, ikiwa ni mwendelezo wa kutekeleza kwa vitendo azma ya serikali kutambua mchango wao na kuwawezesha.
  • Mkutano huo ulifanyika Septemba 19 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri Subira Mgalu, Katibu Mkuu Dkt Hamisi Mwinyimvua, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Leonard Masanja, viongozi pamoja na wataalamu wengine mbalimbali kutoka wizarani na taasisi zilizo chini yake.
2-01
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt Hamisi Miwnyimvua akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati (kulia) na wawekezaji binafsi wa umeme (hawapo pichani), uliofanyika Dar es Salaam, Septemba 19, 2019.
  • Akifungua mkutano huo, Waziri Kalemani alisema serikali itaendelea kutambua na kuthamini mchango wa wazalishaji hao wa umeme na itaendelea kuwajengea mazingira wezeshi ili wakue na kuzalisha zaidi kusudi lengo la kufikia uchumi wa kati na wa viwanda liweze kufikiwa.
  • “Nishati ndiyo injini ya uchumi wa viwanda. Pasipo umeme wa uhakika na wa kutosha, hakuna viwanda. Hivyo basi, pamoja na serikali kuanzisha na kutekeleza miradi mikubwa ya umeme, tungali tunahitaji mchango wenu pia ili tuzalishe umeme wa kutosha kwa ajili ya viwanda na matumizi mengine nchini.”
3-01
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati na wawekezaji binafsi wa umeme (hawapo pichani), uliofanyika Dar es Salaam, Septemba 19, 2019.
  • Aidha, akifunga mkutano husika, Waziri alitaja mambo kadhaa muhimu yatakayozinufaisha pande zote mbili, serikali na wawekezaji kwa kuzingatia manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.
  • Aliwataka wadau wa sekta hiyo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) na wengineo, kupitia upya masharti ya utoaji leseni na kuyaboresha ili kuwajengea wawekezaji mazingira rafiki zaidi ya uwekezaji lakini pasipo kukiuka sheria.
  • Vilevile, Waziri alielekeza kuwa taasisi zinazohusika na utoaji vibali, ziache tabia ya urasimu wa kutumia muda mrefu katika kushughulikia barua za mapendekezo kutoka kwa wawekezaji. Alitaka uwepo utaratibu wa kujibu barua hizo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja lakini kwa kuzingatia sheria.
4-01
Mwakilishi wa wanachama wa Umoja wa Wazalishaji Binafsi wa Umeme Tanzania (Tanzania Independent Power Producers Association – TIPPA), Juma Shamte akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati na wawekezaji binafsi wa umeme (hawapo pichani), uliofanyika Dar es Salaam, Septemba 19, 2019.
  • Aidha, alitoa maelekezo kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kutangaza utaratibu wa upatikanaji ruzuku inayotolewa na serikali kwa wawekezaji hao na kuwashindanisha waombaji kwa uwazi kulingana na sifa zao ili kuepusha upendeleo.
  • Waziri pia alielekeza kwamba maeneo yote mahsusi ya uwekezaji katika sekta ya umeme jadidifu yabainishwe na kuwekwa wazi, ili watu wayajue na kwenda kuwekeza.
  • Kuhusu suala la gharama za umeme, Waziri alielekeza kuwa inapaswa bei zinazotolewa na wawekezaji binafsi ziwiane na za serikali ili kuwawezesha wananchi wote kunufaika na huduma hiyo pasipo malalamiko kuwa wengine wanapendelewa. “Mathalani, gharama iliyowekwa na serikali kuunganisha umeme kwa wananchi vijijini ni shilingi 27,000 tu; nanyi inabidi mjipange ili mtoze bei inayowiana na hiyo,” alisisitiza.
5-01
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt Hamisi Mwinyimvua (kushoto), wakifuatilia hoja zilizokuwa zikiwasilishwa na wawekezaji binafsi wa umeme (hawapo pichani) wakati wa kikao baina yao (wawekezaji) na Waziri kilichofanyika Septemba 19, 2019 jijini Dar es Salaam
  • Kwa upande wake, Naibu Waziri Mgalu aliunga mkono yale yote yaliyoelekezwa na Waziri na akatilia mkazo kuwa taasisi za REA na TANESCO zihakikishe zinaweka utaratibu wa kufanya mapitio ya miradi mbalimbali ya umeme jadidifu inayotekelezwa nchini, hususan katika maeneo ambayo hayafikiwi na gridi ya taifa,  ili kujiridhisha na maendeleo yake.
  • Naye Juma Shamte ambaye ni Mwakilishi wa wanachama wa Umoja wa Wazalishaji Binafsi wa Umeme Tanzania (Tanzania Independent Power Producers Association – TIPPA), alimshukuru Waziri Kalemani na serikali kwa ujumla kwa jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika katika kutambua mchango wao na kuendelea kuwajengea mazingira wezeshi ya uwekezaji.
  • Awali, ilielezwa kuwa hadi sasa, idadi ya wanachama hai waliojiandikisha na kutambulika rasmi na serikali kama wazalishaji binafsi wa umeme nchini, inafikia 110 na kwamba kiasi cha umeme wanachozalisha kinafikia megawati 18 ambapo huingizwa kwenye gridi ya taifa na kiasi kingine hutumika kuhudumia wateja moja kwa moja.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TPDC YAOKOA TRILIONI 12.7 KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa …

16 Maoni

  1. заказать такси по телефону недорого https://zakaz-taxionline.ru/

  2. Портал о Ярославле – ваш гид по культурной жизни города. Здесь вы найдёте информацию о театрах, музеях, галереях и исторических достопримечательностях. Откройте для себя яркие события, фестивали и выставки, которые делают Ярославль культурной жемчужиной России.

  3. Kylian Mbappe https://kylianmbappe.prostoprosport-ar.com is a French footballer, striker for Paris Saint-Germain and captain of the French national team. He began playing football in the semi-professional club Bondi, which plays in the lower leagues of France. He was noticed by Monaco scouts, which he joined in 2015 and that same year, at the age of 16, he made his debut for the Monegasques. The youngest debutant and goal scorer in the club’s history.

  4. Lionel Andres Messi Cuccittini https://lionelmessi.prostoprosport-ar.com is an Argentine footballer, forward and captain of the MLS club Inter Miami, captain of the Argentina national team. World champion, South American champion, Finalissima winner, Olympic champion. Considered one of the best football players of all time.

  5. Ruben Diogo da Silva Neves https://ruben-neves.prostoprosport-ar.com is a Portuguese footballer who plays as a midfielder for the Saudi Arabian club Al-Hilal and the Portuguese national team. Currently, Ruben Neves plays for the Al-Hilal club wearing number 8. His contract with the Saudi club is valid until the end of June 2026.

  6. Lebron Ramone James https://lebronjames.prostoprosport-ar.com American basketball player who plays the positions of small and power forward. He plays for the NBA team Los Angeles Lakers. Experts recognize him as one of the best basketball players in history, and a number of experts put James in first place. One of the highest paid athletes in the world.

  7. Jogo do Tigre https://jogo-do-tigre.prostoprosport-br.com is a simple and fun game that tests your reflexes and coordination. In this game you need to put your finger on the screen, pull out the stick and go through each peg. However, you must ensure that the stick is the right length, neither too long nor too short.

  8. Jamal Musiala https://jamal-musiala.prostoprosport-fr.com footballeur allemand, milieu offensif du club allemand du Bayern et du equipe nationale d’Allemagne. Il a joue pour les equipes anglaises des moins de 15 ans, des moins de 16 ans et des moins de 17 ans. En octobre 2018, il a dispute deux matchs avec l’equipe nationale d’Allemagne U16. En novembre 2020, il a fait ses debuts avec l’equipe d’Angleterre U21.

  9. Kylian Mbappe Lotten https://kylianmbappe.prostoprosport-br.com Futebolista frances, atacante do Paris Saint-Germain e capitao da selecao francesa equipe . Em 1? de julho de 2024, ele se tornara jogador do clube espanhol Real Madrid.

  10. Mohamed Salah https://mohamedsalah.prostoprosport-br.com e um futebolista egipcio que joga como atacante do clube ingles Liverpool e do Selecao egipcia. Considerado um dos melhores jogadores de futebol do mundo. Tricampeao da Chuteira de Ouro da Premier League inglesa: em 2018 (sozinho), 2019 (junto com Sadio Mane e Pierre-Emerick Aubameyang) e 2022 (junto com Son Heung-min).

  11. Ederson Santana de Moraes https://edersonmoraes.prostoprosport-br.com Futebolista brasileiro, goleiro do clube Manchester City e da Selecao Brasileira . Participante do Campeonato Mundial 2018. Bicampeao de Portugal pelo Benfica e pentacampeao de Inglaterra pelo Manchester City.

  12. Neymar da Silva Santos Junior https://neymar.prostoprosport-br.com e um futebolista brasileiro que atua como atacante, ponta e atacante. meio-campista do clube saudita Al-Hilal e da selecao brasileira. Considerado um dos melhores jogadores do mundo. O maior artilheiro da historia da Selecao Brasileira.

  13. Edson Arantes do Nascimento https://pele.prostoprosport-br.com Brazilian footballer, forward (attacking midfielder. Played for Santos clubs) and New York Cosmos. Played 92 matches and scored 77 goals for the Brazilian national team.

  14. Toni Kroos https://toni-kroos.prostoprosport-cz.org je nemecky fotbalista, ktery hraje jako stredni zaloznik za Real Madrid a nemecky narodni tym. Mistr sveta 2014. Prvni nemecky hrac v historii, ktery sestkrat vyhral Ligu mistru UEFA.

  15. Большой выбор игровых автоматов, рабочее зеркало сайта play fortuna зеркало на сегодня играть на реальные деньги онлайн

  16. Pin up entry to the official website. Play online casino Pin Up https://pin-up.prostoprosport.ru for real money. Register on the Pin Up Casino website and claim bonuses!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *