WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI INASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA VIWANDA

  • Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inashiriki katika Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).
  • Kupitia Maonesho hayo, Wananchi wanaelimishwa kuhusu majukumu ya Wizara na utekele zaji wake na namna wizara na balozi za Tanzania zinavyofanya kazi ya kuvutia watalii na wawekezaji kuja nchini kutembelea vivutio vya kitalii na kuwekeza nchini.
1-01
Maafisa wa Wizara wakiwa ndani ya Banda la Wizara tayari kwa ajili ya kuwahudumia wananchi watakaotembelea Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji Biashara Tanzania (TANTRADE) yaliyoanza tarehe 5, Desemba 2019 katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
  • Maonesho hayo ni utekelezaji kwa vitendo  kwa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Viwanda ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2021.
  • Kauli mbiu ya maonesho hayo ya Tanzania sasa Tunajenga Viwanda inalenga kujenga na kuimarisha utamaduni wa Watanzania kutambua, kununua na kuthamini bidhaa zinazozalishwa nchini.
2-01
Afisa wa Wizara akiwa ndanii ya Banda la Wizara tayari kwa ajili ya kuwahudumia wananchi watakaotembelea Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji Biashara Tanzania (TANTRADE) yaliyoanza tarehe 5, Desemba 2019 katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
  • Maonyesho ya Nne ya Viwanda yanahusisha wadau wa Sekta ya Viwanda na yataonesha fursa zilizopo katika katika sekta ya viwanda na yatatoa fursa kwa wadau kuzungumza na kujadili  namna ya kujenga mahusiano endelevu ya biashara.
  • Maonyesho hayo pia yatawezesha kufanyika  kwa mikutano ya wafanyabiashara ambayo itawakutanisha wauzaji na wanunuzi .

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *