KATIBU MKUU NISHATI AKAGUA MITAMBO YA GESI SONGONGO NA MNAZI BAY

  • Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, amefanya ziara ya kikazi katika mitambo ya kuzalisha, kuchakata na kusafirisha gesi asilia iliyopo kisiwani Songo Songo mkoani Lindi, na ile ya Madimba na Mnazi Bay Mkoani Mtwara kwa lengo la kukagua maendeleo ya uzalishaji na uchakataji wa Gesi Asilia katika maeneo hayo.
2-01
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa Tatu kulia), Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi (wa Pili kulia) na Kamishna Msaidizi wa Gesi, Sebastian Shana (wa Tano kutoka kushoto) wakiwa na watendaji wa kampuni ya GASCO na wataalam kutoka Wizara ya Nishati katika mitambo ya Gesi ya Songosongo mkoani Lindi
  • Ziara hiyo aliifanya tarehe 11 Disemba, 2019 akiwa ameambatana na Kamishna wa Gesi na Petroli, Adam Zuberi, Kamishna Msaidizi wa Gesi, Sebastian Shana na watendaji kutoka kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ya GASCO inayoshughulikia masuala ya Usambazaji Gesi .
  • Pamoja na  ukaguzi wa maendeleo ya uzalishaji na uchakataji wa Gesi Asilia katika maeneo hayo, ziara hiyo ililenga kubaini kama kuna changamoto ambazo zinaweza kukwamisha upatikanaji wa Gesi Asilia nchini.
3-01
Mtaalam anayefanya kazi katika mitambo ya kuchakata Gesi Asilia ya Madimba mkoani Mtwara akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (wa Pili kushoto) na wataalam wengine kuhusu kazi zinazofanywa kwenye kituo hicho.
  • Baada ya ukaguzi wa mitambo hiyo, Katibu Mkuu aliwapongeza watendaji wa TPDC na GASCO kwa jinsi walivyoweza kujenga uwezo kwa maafisa wake ambao ndio wanaendesha mitambo hiyo ya  kuchakata Gesi Asilia bila kutegemea wataalam kutoka nje ya nchi.
  • Vile vile, aliwagiza wataalam hao kusimamia vizuri mitambo hiyo ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa Gesi Asilia ambayo inatumika kwa matumizi mbalimbali nchini ikiwemo kuzalisha umeme, kutumika majumbani, viwandani na kwenye magari.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI KALEMANI AFUNGUA KIWANDA CHA NGUZO ZA UMEME – KIGOMA

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amefungua kiwanda cha Nguzo cha Qwihaya, kilichopo katika Mtaa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *