UUNGANISHAJI UMEME VIJIJINI UENDE SAMBAMBA NA IDADI KUBWA YA KUWAWASHIA WATEJA

1-01
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mchangani, katika Kisiwa Kome,wilayani Sengerema mkoani Mwanza alipotembelea kijiji hicho wakati wa kukagua usambazaji wa umeme vijijini.
  • Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amewaagiza Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini(REA) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO)kuwa kasi ya kuunganisha umeme Vijijini iende sambamba na kasi ya kuwawashia Umeme wateja katika Nyumba zao.
  • Mgalu alisema hayo kwa nyakati tofauti alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika Kijiji cha Buchosa na Mchangani Kisiwani Kome wilayani Sengerema, pia katika Kijiji cha Buganda na Dutongo wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Desemba 21 na 22, 2019.
2-01
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( katikati) akipita katika mitaa ya nyumba za wakazi wa Kijiji cha Mchangani, Kisiwani Kome,wilayani Sengerema mkoani Mwanza alipotembelea kijiji hicho wakati wa kukagua usambazaji wa umeme vijijini.
  • Akiwa katika Wilaya hizo, Mgalu alisema kuwa hafurahishwi kuona kasi ndogo ya kuwaunganishia umeme wateja katika vijiji mbalimbali ambavyo tayari vimeunganishwa na umeme,huku kukiwa na wateja wengi wanaohitaji huduma hiyo na tayari wameshalipia.
  • Aidha aliwataka wakandari pamoja na TANESCO kuhakikisha kuwa ndani ya siku saba wawe wamewaunganisha wateja waliolipia, badala ya kuwaacha wateja hao wakisubiri muda mrefu pasipo sababu ya msingi.
3-01
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akikata utepe kuashiria kuwasha umeme katika Kijiji cha Buganda, wilayani Ilemela mkoani Mwanza wakati wa kukagua usambazaji wa umeme vijijini.
  • “Kwakweli haipendezi kuona vijiji vimeunganishwa na umeme, wanaohitaji ni wengi lakini waliowashiwa ni wachache mno, watu wametandaza nyaya katika nyumba zao, na wamelipia lakini hawajawashiwa umeme,bila sababu ya msingi”, alisema Mgalu.
  • Vilevile aliwataka TANESCO kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa wananchi endapo kuna changamoto yoyote inayosababisha mradi kuchelewa ama mtu kutounganishiwa kwa wakati huduma ya umeme ili kuwaondelea hofu wananchi hao na kuwajengea uwezo wa uelewa zaidi namna ambavyo mradi huo unatekelezwa katika maeneo yao.
4-01
aibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akiwasha umeme katika shule ya kijiji cha Dutongo, wilayani Ilemela mkoani Mwanza wakati wa kukagua usambazaji wa umeme vijijini.
  • Akiwa katika Wilaya ya Sengerema, Magalu aliwasha umeme katika Kijiji cha Buchosa na kutembelea Kijiji cha Mchangani kilichopo  katika hifadhi ya Kisiwa cha Kome na kuzungumza na wananchi.
  • Baada ya kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuridhishwa na mazingira ya eneo husika, aliahidi kuwapatia umeme wananchi hao waliokuwa wakiusubiri kwa muda mrefu baada ya kufanya mazungumzo na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuona namna bora ya kufikisha huduma hiyo eneo hilo.
5-01
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Buganda,wilayani Ilemela mkoani Mwanza wakati wa kukagua usambazaji wa umeme vijijini.
  • Wakazi wa eneo hilo awali walitakiwa kuondoka eneo kupisha eneo la hifadhi katika Kijiji hicho na hawakuwa wakipatiwa huduma muhimu stahiki ikiwemo umeme kwa kile kinachoelezwa kuwa wamevamia eneo la hifadhi, na kufanya shughuli za uvuvi na biashara mbalimbali.
  • Hata hivyo uomgozi wa Kijiji ulimueleza Mgalu kuwa. Wizara yenye dhamana ya kusimamia hifadhi hiyo imetoa kibali cha kuwaruhusu wananchi hao kuendelea kuishi eneo hilo kwa sharti la kutojenga nyumba za kudumu, kulinda na kutunza hifadhi hiyo wakati wakiendelea na shughuli zao.
6-01
Mbunge wa Jimbo la Buchosa,Charles Tizeba akuzungumza na wakazi wa eneo hilo, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wilayani Sengerema mkoani Mwanza wakati wa kukagua usambazaji wa umeme vijijini.
  • Katika Wilaya ya Ilemela, Mgalu aliwasha umeme katika Kijiji Buganda na Dutongo, ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wananchi kuendelea kulipia gharama za kuunganishiwa umeme ya shilingi 27,000 tu, pia wasikubali kutozwa gharama za nguzo, nyaya wala mita kwakuwa gharama hizo zimegharamiwa na serikali.
  • Pia aliwaeleza kuwa hakuna kiijiji wala kaya itakayorukwa wala kuachwa kuunganishiwa umeme, wawe na subira kwa kuwa watapatiwa umeme.Na Zuena Msuya, Mwanza
Ad

Unaweza kuangalia pia

TPDC YAOKOA TRILIONI 12.7 KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *