Maktaba ya Mwaka: 2019

MAENDELEO YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA UYUI, KUMALIZIKA MWEZI JUNI

Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Uyui unatarajia kukamilika mwishoni mwa Mwezi ujao tayari kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi. Kauli hiyo imetolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati akielezea maendeleo ya ujenzi wa majengo saba ya Hospitali hiyo. Alisema kwa upande wa jengo …

Soma zaidi »

MARUFUKU AJIRA KWA WATOTO KWENYE SEKTA YA TUMBAKU – WAZIRI HASUNGA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesisitiza agizo lake alilolitoa hivi karibuni kuhusu ajira kwa watoto ambao wapo chini ya miaka 18. Mhe Hasunga amepiga marufuku kitendo hicho tarehe 13 Mei 2019 wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya Tumbaku katika hafla ya ufunguzi wa msimu wa masoko ya Tumbaku …

Soma zaidi »

MKANDARASI ASAINI MKATABA MRADI WA MAJI NYASHIMO WILAYANI BUSEGA

Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) imesaini mkataba na mkandarasi kampuni ya BENNET Contractors, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji kwa wakazi wa Kata ya Nyashimo, Wilaya Busega mkoani Simiyu. Mkataba huo umesainiwa Mei 10, 2019 na kushuhudiwa na wananchi pamoja …

Soma zaidi »

SERIKALI YATEKELEZA AHADI YA KUPELEKA UMEME KWA WACHIMBAJI WADOGO NYAKAFURU

Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imetekeleza ahadi ya kupeleka umeme kwenye migodi ya wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Nyakafuru wilayani Mbogwe hivyo kuwawezesha wachimbaji hao kutumia umeme badala ya mafuta katika kuendesha mitambo mbalimbali ikiwemo ya kuchenjulia madini. Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani aliwasha umeme …

Soma zaidi »

SOKO LA MIANZI NI KUBWA SANA DUNIANI – BALOZI MCHUMO

Shirika la Kimataifa la Kuendeleza na Kusimamia Biashara ya Mianzi (INBAR) limesema ipo haja kwa Serikali ya Tanzania kutunga Sera zitakazoweza kuhamasisha wakulima hapa nchini kulima zao hilo ambalo pamoja na kuhifadhi Mazingira pia lina tija kiuchumi. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam jana Jumamosi (Mei 11, …

Soma zaidi »