MKANDARASI ASAINI MKATABA MRADI WA MAJI NYASHIMO WILAYANI BUSEGA

WAKAZI
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Nyashimo wilayani Busega wakifuatilia zoezi hilo.
  • Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) imesaini mkataba na mkandarasi kampuni ya BENNET Contractors, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji kwa wakazi wa Kata ya Nyashimo, Wilaya Busega mkoani Simiyu.
VIONGOZI
Viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (wa pili kushoto) wakiwa kwenye zoezi hilo.
  • Mkataba huo umesainiwa Mei 10, 2019 na kushuhudiwa na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka aliyebainisha kwamba kukamilika kwa miradi mbalimbali ya maji wilayani Busega, kutaongeza idadi wananchi wanaofikiwa na mtandao wa maji safi na salama kutoka asilimia 39 za sasa hadi asilimia 79.
MKUU WA MKOA
Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka akizungumza kwenye zoezi hilo la kusaini mkataba wa mradi wa maji Nyashimo wilayani Busega.
  • Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga amesema utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 ni sehemu ya ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Nyashimo.
MKATABA
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya BENNET Contractors, Sabatho Boaz (kulia) wakisaini mkataba wa utekelezaji mradi wa maji ya bomba katika Nyashimo wilayani Busega. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka.
  • Naye Mkurugenzi wa kampuni ya BENNET Contractors, Sabatho Boaz ameahidi kukamilisha mradi huo kwa ubora na kwa muda wa miezi 15 kama mkataba unavyoelekeza ili kuwaondolea wananchi wa Kata ya Nyashimo adha ya upatikanaji wa maji safi na salama.Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Ad

Unaweza kuangalia pia

MIRADI YA MAJI 547 INATEKELEZWA KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI – PROF MBARAWA

Jumla ya miradi ya maji 547 inaendelea kutekelzwa nchini yenye thamani ya shilingi trilion 3.76, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *