WAZIRI JAFO ATAKA MACHINJIO YA KISASA YA KIZOTA KUREKEBISHA CHANGAMOTO ZAO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo ameupa uongozi wa machinjio ya kisasa ya Kizota jijini Dodoma miezi sita kurekebisha changamoto ya utiririshaji wa majitaka ovyo.

Jafo ametoa agizo hilo leo Aprili 8, 2021 alipofanya ziara ya kikazi katika machinjo hiyo kwa ajili ya kukagua udhibiti wa majitaka na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.

Ad
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kukagua utuzanjaji mazingira alipofanya ziara ya kikazi katika kiwanda cha kurejeleza taka za plastiki cha Future Colorful Limited kikichopo Kizota jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelezo kuhusu utendaji wa machinjio ya kisasa kutoka kwa Meneja wa machinjio hayo katika eneo la Kizota jiji Dodoma Chacha Mwita alipofanya ziara ya kikazi kukagua utunzaji wa mazingira machinjioni hapo.

Alisema kuwa kila kiwanda lazima kiwe na mpango wa namna ya kuyatibu majitaka na kudhibiti utiririshaji wake kuepusha yasiende kwenye makazi yao watu na kusababisha madhara ya kiafya.

“Nafahamu machinjio hii ni miongoni mwa machinjo kubwa na ina soko kubwa katika nchi za Mashariki ya Kati wananunua nyama nami nimekuja hapa kujiridhisha kuhusu suala zima la utiririshaji wa majitaka,” alisema.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kukagua utuzanjaji mazingira alipofanya ziara ya kikazi katika kiwanda cha kurejeleza taka za plastiki cha Future Colorful Limited kikichopo Kizota jijini Dodoma. Kushoto ni Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Kati Flanklin Rwezimula na mmiliki wa kiwanda hicho Wang Zuo Min.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelezo kuhusu utendaji wa machinjio ya kisasa katika eneo la Kizota jiji Dodoma alipofanya ziara ya kikazi kukagua utunzaji wa mazingira machinjioni hapo.

Alimuelekeza Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Kati Flanklin Rwezimula kufuatilia kazi ya kuhakikisha machinjio hiyo inatengeneza mfumo wa kutibu majitaka haraka.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *