SERIKALI KUIDHINISHA KIASI CHA BILIONI 372.34 KWA AJILI YA KUANZA UJENZI WA KIPANDE CHA 5 CHA RELI YA MWANZA – ISAKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 22 Mei, 2021 amezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Masanja Kadogosa kuhusu maendeleo ya miradi ya ujenzi wa reli na maendeleo ya TRC.

Katika mazungumzo hayo, Bw. Kadogosa amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa Serikali ya Awamu ya Sita kuidhinisha kiasi cha shilingi Bilioni 372.34 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kipande cha 5 cha reli ya Mwanza – Isaka chenye urefu wa kilometa 341 kwa kiwango cha kisasa (standard gauge railways).

Ad

Bw. Kadogosa ameeleza kuwa tangu Mhe. Rais Samia aingie madarakani ujenzi wa reli katika vipande 2 unaendelea vizuri ambapo hadi mwezi uliopita kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (kilometa 300) kilikuwa kimefikia ya asilimia 91 na Morogoro – Makutupora (kilometa 422) kilikuwa kimefikia asilimia 60.02.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa akizungumza na Wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Amebainisha kuwa majaribo ya treni ya abiria yanatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti, 2021 kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro.

Kwa upande wake, Mhe. Rais Samia amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuhakikisha ujenzi wa reli ya kati utakaounganisha Bandari ya Dar es Salaam na Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi unakamilishwa ili kuzifikia nchi za Uganda, Burundi, Rwanda na DRC.

Amemtaka Bw. Kadogosa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ya ujenzi vizuri ikiwa ni pamoja na kujipanga kwa ajili ya ujenzi wa vipande vya Makutopora – Tabora, Tabora – Isaka na Kaliua – Mpanda – Kalema.

Mhe. Rais Samia ameipongeza TRC chini ya Bw. Kadogosa pamoja na wote wanaoshiriki katika ujenzi wa reli kwa kazi nzuri wanayoifanya na ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya miradi hiyo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *