RAIS MAGUFULI AWASILI NCHINI ZIMBABWE KWA ZIARA RASMI YA KITAIFA YA SIKU 2

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2019 amewasili katika Jiji la Harare nchini Zimbabwe ambapo anafanya Ziara Rasmi ya Kitaifa ya siku 2 kwa mwaliko wa Rais wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa.
  • Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Mugabe, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa rasmi na mwenyeji wake, Mhe. Rais Mnangagwa kisha kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na kupigiwa mizinga 21.
RAI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2019 amewasili katika Jiji la Harare nchini Zimbabwe ambapo amepokelewa na mwenyeji wake mwaliko wa Rais wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa.
  • Baadaye leo, Mhe. Rais Magufuli atakuwa na mazungumzo ya falagha na mwenyeji wake, Mhe. Rais Munangagwa na kisha atahudhuria Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Mhe. Rais Mnangagwa kwa heshima yake.
  • Kesho, Mhe. Rais Magufuli atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake na kisha atatembelea na kuweka shada la maua katika eneo la mashujaa wa ukombozi wa Zimbabwe.
  • Katika ziara hii Mhe. Rais Magufuli ameongozana na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndg. Philip Mangula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *