Taarifa Vyombo vya Habari

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAPONGEZWA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA

Serikali imesema itaendelea na juhudi za kushawishi wadau wa maendeleo na Jumuiya za Kimataifa ili kupata fedha za kusimamia uratibu wa shughuli za mazingira na kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi nchini. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba ameyasema hayo hii leo …

Soma zaidi »

WIZARA ITAENEDLEA KUANZISHA MASOKO YA MADINI – WAZIRI BITEKO

Wizara ya Madini itaendelea kusimamia Uanzishwaji wa Masoko ya Madini katika maeneo mbalimbali nchini huku ikiendelea kufanya marekebisho ya Kanuni za Uanzishwaji wa masoko hayo. Waziri wa Madini Doto Biteko ameyasema hayo Machi 31, 2019 wakati akifunga Semina ya siku mbili iliyoandaliwa na wizara kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu …

Soma zaidi »

MRADI WA MAJI MLANDIZI MBOGA KUANZA KATIKATI YA MWEZI WA NNE

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ametembelea kiwanda cha mabomba cha Tanzania Steel Pipes kinachotengeneza mabomba ya kusafirishia maji kwenye mradi wa maji wa Mlandizi- Chalinze- Mboga, ambapo takribani mabomba 321 yameanza kusafirishwa kwa ajili ujenzi wa mradi huo unaotarajiwa kuanza katikati ya mwezi April. Amesema, kukamilika kwa mradi huo ambao …

Soma zaidi »

UTOAJI WA ELIMU BORA NI KIPAUMBELE CHA NCHI – WAZIRI MKUU MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema utoaji wa elimu bora kwa Watanzania ni moja ya vipaumbele vya nchi katika kuleta maendeleo na kufikia malengo ya Milenia 2025, Elimu kwa wote (EFA) na Mkakati wa Kupambana na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA). Amesema ili kuweza kufanikisha malengo hayo wanahitaji sekta hiyo kuwa bora, …

Soma zaidi »

PROF PALAMAGAMBA AKUTANA NA BARONESS LYNDA CHALKER

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amesema mabadiliko yote ya sheria yaliyofanyika hivi karibuni katika sekta za madini,maliasili na uwekezaji yana lengo la kuweka mazingira bora zaidi yatakayoleta tija kwa Taifa na wawekezaji kutokana  na sheria mpya kuondoa utaifishaji (nationalization) na upokonyaji …

Soma zaidi »

WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2018 RUKSA KUBADILISHA TAHSUSI(COMBINATION)

Serikali imetoa fursa kwa wanafunzi waliofaulu kidato cha nne mwaka 2018 na wanaotegemea kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo kwa mwaka 2019 kubadilisha Tahsusi(Combination). Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo Serikali ya …

Soma zaidi »

MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO NA MASHINE ZA TIBA ZA LINAC KATIKA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la saratani kwa Watanzania linaweza kupungua ama kuondokana nalo endapo kutakuwa na tabia ya kupima afya zetu mara kwa mara. Makamu wa Rais ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa jengo na mashine mpya za tiba …

Soma zaidi »

MAKAMU WA RAIS AZINDUA TABASAMU AKAUNTI MAALUM KWA AJILI YA WANAWAKE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano imefanya jitihada kubwa kuweka mazingira mazuri ya kisera na kimifumo ili kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha hapa nchini. Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Akaunti …

Soma zaidi »