WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2018 RUKSA KUBADILISHA TAHSUSI(COMBINATION)

  • Serikali imetoa fursa kwa wanafunzi waliofaulu kidato cha nne mwaka 2018 na wanaotegemea kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo kwa mwaka 2019 kubadilisha Tahsusi(Combination).
  • Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo Serikali ya Awamu ya Tano inawapa wahitimu hao fursa ya kufanya mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi (Combination) na kozi mbalimbali walizozichagua kwenye fomu ya “F4-Selform.
  • Amesema Fursa hii itawawezesha wanafunzi kurekebisha machaguo yao kulingana na ufaulu waliopata kwenye matokeo ya Kidato cha Nne 2018 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania, NECTA.
  • “Kwa mara ya kwanza Wanafunzi watakuwa na uwezo wa kubadili machaguo au kuchagua kutoka Kidato cha Tano kwenda Chuo au Chuo kwenda Kidato cha Tano kwa kadiri ya mahitaji yake na jinsi alivyofaulu mitihani yake” alisema Jafo.
  • Unajua wanafunzi hujaza Fomu za F4-Selform kabla ya kufanya mitihani sasa matokeo huweza kuja tofauti na vile alivyojaza lakini mwanafunzi huyo amefaulu hivyo ni wakati sasa kwa kubadilisha machaguo kwa kadiri ya ufaulu wake na anavyopendelea mwenyewe alisisitiza Jafo.
  • Aidha Waziri aliongeza kuwa Ofisi yangu imetoa fursa hii kwa wahitimu kubadili machaguo yao ili kutoa mwanya zaidi kwa mwanafunzi kusoma fani au Tahasusi itakayomwandaa kuwa na mtaalam fulani katika maisha yake ya baadaye kwa namna ambayo anatamani yeye mwenyewe au kwa kushauriwa na wazazi au walezi wake; Hii ni kutokana na ukweli kwamba baadhi ya wanafunzi hawakujaza kwa uhakika Tahasusi au Kozi zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu katika masomo yao.
  • Aliongeza kuwa zoezi la awali la kuingiza taarifa zilizo kwenye “Selform” za wanafunzi kwenye kanzidata ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI, kama zilivyojazwa wakiwa shuleni kabla ya kuhitimu limekamilika na sasa wanafunzi wataweza kufanya mabadiliko kwa njia ya mtandao, (online) na baada ya wanafunzi kufanya marekebisho yao, kanzidata hii ndiyo itakayotumika kuwachagua na kuwapangia kidato cha Tano na Kozi za Vyuo.
  • Waziri Jafo aliwakumbusha wahitimu wote  kuwa, endapo wanapenda kurekebisha machaguo ya Tahasusi na Kozi au kuhama kutoka Chuo kwenda Kidato cha Tano kulingana na ufaulu wao katika masomo wanatakiwa kuingia kwenye mfumo wa Selform unaopatikana katika anuani ya www.selform.tamisemi.go.tz na   maelekezo ya jinsi ya kufanya mabadiliko watayapata kwenye video ya mafunzo  inayopatikana kwenye tovuti ya TAMISEMI www.tamisemi.go.tz
  • Pia alifafanua kuwa Ili mhitimu aweze kuingia kwenye mfumo itabidi kutumia namba ya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 2018, jina lake la mwisho, mwaka wa kuzaliwa na alama ya ufaulu aliyopata kwenye somo atakaloulizwa na mfumo au swali lolote atakaloulizwa.
  • Zoezi hili la kubadilisha Tahasusi litafanyika kuanzia tarehe 01/04/2019 hadi tarehe 15/04/2019.
Ad

Unaweza kuangalia pia

KINONDONI YA TUMIA BILIONI 1.5 UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi …

2 Maoni

  1. Fortunatus Simfukwe

    Pongezi sana kwa serikali, kutokana na kwamba wanafunzi katika level ya kidato cha nne in vigumu sana kuwa na kombi maalumu, kwani while nyingi zinafundisha masomo yote ya sayansi na Art, hivyo humpa mwanafunzi wakati mgumu kuamua kuchagua kombi anayoitaka kwakuwa bado anakuwa dilemma kujua ni masomo yepi hasa anayamudu.

    Agharabu ni wanafunzi wachache sana wanaweza kujitambua na kuchagua kombi wanazozitaka, wengi huwa inakuja tu mshangao somo ambalo hakutegemea kufaulu ndiyo kafaulu vizuri kuliko kombi aliyochagua, hivyo kwangu binafsi naunga mkono na kupongeza kitendo cha serikali kuliona hilo na kuwapa watoto fursa ya kubadili kombi zao,
    Congole sana Mhe. Jafo.
    Congole waziri wa Elimu Mhe. Prof: Ndalichako

  2. Mambo ni mazuri kwa kweli hii ni furasa nyingine kwenu vijana jitihada hizi zimelenga kukukomboa wewe muhim hapa chukua hatua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *