MRADI WA MAJI MLANDIZI MBOGA KUANZA KATIKATI YA MWEZI WA NNE

  • Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ametembelea kiwanda cha mabomba cha Tanzania Steel Pipes kinachotengeneza mabomba ya kusafirishia maji kwenye mradi wa maji wa Mlandizi- Chalinze- Mboga, ambapo takribani mabomba 321 yameanza kusafirishwa kwa ajili ujenzi wa mradi huo unaotarajiwa kuanza katikati ya mwezi April.
  • Amesema, kukamilika kwa mradi huo ambao wameahidi utakuwa umekamilika katika kipindi cha miezi mitano hadi sita utasaidia kutatua tatizo la maji katika eneo kubwa la Chalinze.
RIDHIOWANI
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa ndani ya gari lililobeba mabomba yanayoelekea kwenye jimbo lake kwa ajili ya mradi wa maji wa Mlandizi Mboga baada ya kutembelea kiwanda cha Mabomba cha Tanzania Steel Pipes leo Jijini Dar es Salaam.
  • “Sikuwahi kuona namna wananchi wanatumia maji pamoja na wanyama kama ng’ombe ila kukamilika kwa mradi huu kutawezesha watu wangu kupata majisafi na salama ila na wao kwa upande wao nitawaomba walipie huduma ili kuweza kuendesha miradi hii maji yaweze kupatikana,”amesema Ridhiwani.
  • Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa DAWASA Mhandisi Aron Joseph amesema mradi huo utawanufaisha wakazi wa maeneo hayo ikiwa pamoja na wananchi wanaoishi kwenye eneo la mradi.

RIDHIWANI

  • Joseph amesema Mradi wa maji wa Mlandizi -Mboga unatarajiwa kusafirisha maji lita milioni 9.3  (mita za ujazo 9300) kwa siku kiasi kianchokisiwa kuweza kutosheleza mahitaji ya walengwa kwa sasa na ongezeko la matumizi kwa siku za usoni.
  • “Hadi sasa, kiasi cha mabomba ya umbali wa km 3.7 yameshazalishwa katika kiwanda cha TSP na yameanza kupelekwa kwenye maeneo ya mradi ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza katika Vijiji vya Mboga na Msoga,” amesema Joseph.
RIDHI-4
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa anakagua eneo lilalotengenezwa mabomba ya kusambazia maji yatakayotumika kwenye mradi wa maji Mlandizi Mboga leo Jijini Dar es Salaam.
  • “Katika usanifu wa mradi huo, umetilia maanani ongezeko la watu na mahitaji ya miaka 20 ijayo na kutosheleza idadi ya watu hadi kufikia 120,912 ndani ya eneo la mradi na utakuwa kwa umbali wa Kilomita 58 ujenzi wa vituo viwili vya kusukumia maji na utagharimu bilion 14 hadi kukamilika kwake,”amesema Joseph.
  • Afisa Utawala wa Kiwanda cha Mabomba cha TSP, Elly Bohela amesema anashukuru sana kwa Mbunge Ridhiwani Kikwete kufika kwenye Kiwanda chao kuona namna wanavyotengeneza mabomba hayo ambayo yanaenda kuwekwa kwenye mradi uliopo katika jimbo lake.
RIDHIWANI
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa anakagua eneo lilalotengenezwa mabomba ya kusambazia maji yatakayotumika kwenye mradi wa maji Mlandizi Mboga leo Jijini Dar es Salaam.
  • Amesema, kiwanda cha TSP ni cha wazawa na wamejizatiti kwenye kutengeneza mabomba yenye ubora aidha ameishukuru dawasa kwa kuweza kuwaamini na kuwapatia kazi hiyo muhimu.
RIDHIWANI
Mbunge wa Chalinze akielezea kwa umakini ramani ya mradi wa Mlandizi Mboga unaotarajiwa kuanza kujengwa Katikati ya mwezi April mwaka huu utakaohudumia wakazi wa jimboni kwake akiwa sambamba na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Arone Joseph na Mkurugenzi wa Miradi DAWASA Mhandisi Lydia Ndibalema.
  • Maeneo yatakayohudumiwa na mradi huo ni pamoja na Ruvu darajani, Vigwaza,Ranchi ya Taifa Ruvu (NARCO), Chahua -Lukenge, Visenzi, Buyuni na Mdaula -Unebazomozi.
  • Kwingine ni Chamakweza, Pingi, Pera, Chalinze, Chalinze Mzee, Msoga na Mboga aidha, viwanda vitakavyofaidika ni pamoja na Twyford, kiwanda cha ngozi, kiwanda cha Matunda cha Sayona pamoja na watumiaji wengine wakubwa ikiwemo kampuni Yapi Merkezi wajenzireli ya kisasa (SGR)
Ad

Unaweza kuangalia pia

TUMEDHAMIRIA KUONGEZA WIGO UPASUAJI – DKT. KAJUNGU

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mkoani kilichopo mkoani Pwani katika Halmashuri ya Kibaha Mji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *