MAKAMU WA RAIS AZINDUA TABASAMU AKAUNTI MAALUM KWA AJILI YA WANAWAKE

  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano imefanya jitihada kubwa kuweka mazingira mazuri ya kisera na kimifumo ili kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha hapa nchini.
MAKAMU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Dkt. Edmund Mndolwa (kulia) wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  • Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Akaunti ya TABASASMU, iliyozinduliwa leo na Benki ya Posta jijini Dar es Salaam.
  • “Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania imeendelea kutoa miongozo mbalimbali ili kuhakikisha watanzania takribani asilimia 50 wanafikiwa na huduma za kibenki ifikapo Mwaka 2025”alisema Makamu wa Rais.
MAKAMU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam.
  • Makamu wa Rais amependezwa na wazo la kuhakikisha kuwa kupitia akaunti ya TABASAMU wanawake watauziwa bima za kijamii.
  • Benki ya Posta ina matawi takriban 80, ATM 54, mtandao wa Umoja Switch takriban 200 na mawakala 150 kupitia Shirika la Posta ambapo Makamu wa Rais ameitaka benki hiyo kuwafikia wanawake wengi haswa vijijini na kuhakikisha wanapata huduma na elimu ya masuala ya kifedha.
MAKAMU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Dkt. Edmund Mndolwa (kulia) wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam.
  • Makamu wa Rais amesisitiza kuwa wanawake ni nguzo kuu ya uchumi wetu, kwani wao ndiyo wazalishaji wakuu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa. Mbali ya kulea familia, huwezi kuwakosa wanawake kwenye sekta yoyote ya uzalishaji mali, na hivyo siyo upendeleo kuanzisha akaunti maalumu ya TABASAMkwa wanawake, bali ni haki yao ya msingi kama ilivyofanya benki ya TPB.
TPB-5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa  na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Dkt. Edmund Mndolwa (kulia) wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam. 
  • Makamu wa Rais amewataka Akaunti ya TABASAM inashirikiana na makampuni ya simu kuhakikisha kuwa wanawake hawa si tu wanapata taarifa za kibenki hata ikiwezekana kuweza kupata huduma za kibenki kama mikopo kupitia simu zao za mikononi.
TPB-6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam.
  • Wakati huo huo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema Tanzania ina rekodi nzuri Afrika na duniani kwa ujumla katika masuala ya huduma za kifedha
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI KUENDELEA KUCHUKUA HATUA KWA WAZALISHAJI NA WASAMBAZAJI WA MIFUKO ISIYOKIDHI VIWANGO – WAZIRI ZUNGU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *