WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AUAGIZA UONGOZI WA WILAYA YA ILEMELA KUHAKIKISHA HOSPITALI MPYA YA WILAYA INATOA HUDUMA KIKAMILIFU

Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Mwanza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Mwanaidi Ali Khamis, amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilemela kuhakikisha vifaa tiba, umeme na maji vinapatikana kwa haraka katika Hospitali mpya ya Wilaya hiyo iliyojengwa katika eneo la Kabusungu  ili huduma za afya zianze kutolewa …

Soma zaidi »

DKT. MPANGO AAGIZA WATUMISHI 22 TRA WASIMAMISHWE KAZI

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, amemwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Dkt. Edwin Mhede kuwasimamisha kazi watumishi 22 wa Mamlaka hiyo wakiwemo baadhi ya Maneja wa TRA wa Mikoa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili za kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kujihusha na …

Soma zaidi »

SERIKALI YASAINI MKATABA NA KOREA UTAKAOWEZESHA TANZANIA KUPATA MIKOPO YENYE MASHARTI NAFUU

Balozi wa Korea nchini, Cho Tae-Ick akizungumza baada ya kusaini mkataba huo baina ya nchi yake na Serikali ya Tanzania leo jijini Dodoma. Serikali ya Tanzania imesaini mkataba na Serikali ya Jamhuri ya Korea utakaowezesha kupata mikopo kutoka mfuko wa ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi wa Korea (EDCF). Mkataba huo …

Soma zaidi »

TANZANIA YAIPONGEZA AfDB KWA KUENDELEA KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango(kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), nchini Dkt. Alex Mubiru (kushoto), alipokuwa akimuaga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi katika Ofisi ya Rais wa Benki hiyo makao makuu Jijini …

Soma zaidi »

DKT. MPANGO AWAASA MADIWANI NCHINI KUSIMAMIA VIZURI MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI

Na Benny Mwaipaja, Kigoma WAZIRI wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma, Dkt. Philip Isdor Mpango, ameyaagiza mabaraza ya Madiwani kote nchini, kuhakikisha kuwa fedha za miradi zinazotumwa na Serikali katika maeneo yao zinasimamiwa vizuri ili kuleta tija na maendeleo ya jamii Dkt. …

Soma zaidi »

BENKI YA NMB YAZINDUA ATM YA KWANZA YENYE UWEZO WA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI NCHINI

Benki ya NMB imezindua mashine ya kutolea fedha (Automated Teller Machine – ATM) ya kwanza nchini Tanzania yenye uwezo wa kubadili fedha za kigeni kwenda shilingi za kitazania. Hatua hiyo imetajwa kuwa ni muhimu kwa Benki ya NMB ya utoaji huduma kwa Watanzania wanaosafiri kwenda nje na watalii wanaokuja nchini …

Soma zaidi »

DKT. MPANGO AWAAGIZA WATENDAJI WA WIZARA KUCHAPAKAZI KWA BIDII ZAIDI

Na. Peter Haule na Farida Ramadhani, Dodoma Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewataka watumishi wa Wizara yake kuhakikisha wanasimamia kikamilifu mapato na matumizi ya fedha za umma ili kufanikisha malengo ya maendeleo yaliyotolewa na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, akizindua Bunge la 12. Hayo aliyasema wakati …

Soma zaidi »

VIWANJA VYA NDEGE VYA SHINYANGA, KIGOMA, TABORA NA SUMBAWANGA KUJENGWA KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Na. Ramadhani Kissimba na Peter Haule, Dar es Salaam Serikali imezindua mradi wa ujenzi, ukarabati na upanuzi wa viwanja vinne vya ndege vya Shinyanga, Tabora, Sumbawanga na Kigoma ili viwe na kiwango cha kimataifa, utakaogharimu shilingi bilioni 136.85. Akizindua ujenzi wa mradi huo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa …

Soma zaidi »

USWISS YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 44.1 KWA AJILI YA KUONDOA UMASIKINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Balozi wa Uswiss nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot,wakionesha Mikataba miwili ya msaada wa Faranga za Uswis milioni 17.8 sawa na Sh. bilioni 44.1 kwa ajili ya kugharamia Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) …

Soma zaidi »

DOTO JAMES: MIRADI YA KIMKAKATI INAYOTEKELEZWA NCHINI NI KWA MUJIBU WA SHERIA

Na. Farida Ramadhani na Ivona Tumsime, WFM, Dodoma Serikali imesema kuwa miradi yote mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa nchini imeshapangwa ndani ya bajeti za kisekta za Wizara husika ambazo hupitishwa na Bunge kila mwaka. Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James wakati wa ufunguzi …

Soma zaidi »