DKT. MPANGO AWAAGIZA WATENDAJI WA WIZARA KUCHAPAKAZI KWA BIDII ZAIDI

Na. Peter Haule na Farida Ramadhani, Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewataka watumishi wa Wizara yake kuhakikisha wanasimamia kikamilifu mapato na matumizi ya fedha za umma ili kufanikisha malengo ya maendeleo yaliyotolewa na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, akizindua Bunge la 12.

Ad

Hayo aliyasema wakati akipokelewa katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba Jijini Dodoma baada ya kuteuliwa na kuapichwa na Mhe. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushika wadhifa wa Waziri wa Fedha na Mipango kwa mara ya pili, Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Isdor Mpango (Mb) akinyanyua ua kwa furaha baada ya kukabidhiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mary Maganga (wa pili kushoto), baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali-Mtumba, baada ya kuapichwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Michael John.

Dkt. Mpango alisema kuwa bado kuna shida kubwa  katika eneo la matumizi ya fedha za umma, kwa kuwa fedha zinazopelekwa kutekeleza miradi mbalimbali hazitumiwi vizuri na kusababisha miradi mingine kutekelezwa chini ya kiwango.

“Tunahitaji jicho la pekee katika Halmashauri za Wilaya na Miji, tunapeleka fedha za miradi lakini mimi nakadiria kuna upotevu wa takribani asilimia arobani ya fedha hizo kwahiyo ni lazima tuwe na jicho kali ili kuokoa fedha za wananchi”, alieleza Dkt. Mpango.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Isdor Mpango (Mb) (kulia), akipokelewa kwa furaha na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James, baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba, baada ya kuapichwa na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Ikulu, Chamwino jijini Dodoma, kushika wadhifa huo kwa awamu nyingine.

Dkt. Mpango alisema mpango wa kununua Ndege, Meli na vitu vingine katika kipindi cha miaka mitano itafanikiwa iwapo kila mmoja katika nafasi yake atasimama imara kuhakikisha mapato yanakusanywa na yanatumika kikamilifu.

Alisema kuwa Watanzania wanamatarajio makubwa kutoka katika Serikali yao hivyo watumishi wa Wizara ambao ni kama kitovu cha maendeleo wanatakiwa kuhakikisha matarajio hayo yanafikiwa.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na watumishi wa Wizara hiyo, baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba, baada ya kuapichwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Dkt. Mpango amewashukuru Watumishi wa Wizara yake kwa utendaji kazi mzuri kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita lakini ameomba waongeze jitihada na maarifa katika kutekeleza miongozo mbalimbali ikiwemo Hotuba ya Rais ya kufungua Bunge la 12, Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuweka mikakati Madhubuti ya kufanikisha utekelezaji wake.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, alimhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango kwamba Menejimenti imejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa inaendelea kutoa ushauri wa kitaalam ili nchi iweze kufikia malengo iliyojiwekea katika kukuza uchumi.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa Wizara hiyo, baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba, baada ya kuapichwa na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM-DODOMA.)

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *