Recent Posts

Malezi bora ni msingi muhimu kwa taifa imara, na Katiba ya Tanzania inaweka misingi ya kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi. Kifungu cha 11 cha Katiba kinatamka kuwa kila mtu ana haki ya kupata elimu. Kwa hivyo, kuhakikisha watoto wanapata elimu bora ni kutimiza hitaji la kikatiba.

Aidha, Katiba inasisitiza maadili na uzalendo. Malezi bora yanajumuisha kuwafundisha watoto maadili mema, heshima, na upendo kwa taifa lao. Kwa kuwalea watoto katika mazingira yenye maadili mema na kuwapatia elimu bora, tunawaandaa kuwa raia wema na wenye uzalendo wa kweli. Hii inasaidia kujenga taifa lenye umoja, amani, na maendeleo. #SisiNdioWajenziWaTanzaniaYetu …

Soma zaidi »

Meli tatu za kivita za Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China  zimewasili katika Bandari ya Dar es Salaam zikiwa na wanajeshi kadhaa kwa ajili ya kushiriki mazoezi ya pamoja na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ikiwa ni sehemu  maadhimisho miaka 60 ya Jeshi hilo na ushirikiano kati ya Nchi ya Tanzania na China tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza Julia 24, 2024 katika Bandari ya Dar es Salaam wakati akipokea Meli tatu za Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji Tanzania NAVY, Rear Admiral Ameir Ramadan Hassan, amesema kuwa  ujio wa meli hizo kutoka Jamhuri ya Watu wa China ni sehemu …

Soma zaidi »