Maktaba Kiungo: UMEME VIJIJINI

WANANCHI VIJIJINI RUKSA KULIPIA UMEME KWA KUDUNDULIZA

Wananchi wa maeneo ya vijijini ambao hawana uwezo wa kulipia shiingi 27,000 za kuunganishiwa umeme kwa mkupuo, sasa wanaweza kulipia huduma hiyo kwa kudunduliza kidogo kidogo. Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani aliyasema hayo Disemba 3, 2019 kijijini Mnekezi, wilayani Chato, ambapo alikuwa akizungumza na wananchi kabla ya kuwasha rasmi …

Soma zaidi »

TANZANIA NA NAMIBIA WAJADILIANA KUHUSU SACREEE

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Naibu Waziri wa Nishati wa Namibia, Kornelia Shilunga pamoja na ujumbe wake, wamekutana na kujadili kwa pamoja kuhusu Kituo cha Nishati Jadidifu na matumizi bora ya Nishati cha nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SACREEE). Mgalu alikutana na ujumbe huo, Desemba 2, 2019, uliofika …

Soma zaidi »

DKT KALEMANI ATAKA TANESCO IFANYE KAZI KAMA KAMPUNI ZA SIMU

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewaagiza mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwafuata wamiliki wa viwanda, migodi ya madini na hoteli kuwashawishi watumie umeme ili kuzalisha kwa tija hali itakayolipatia shirika hilo mapato zaidi kutokana na malipo ya umeme. Akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ofisini kwa …

Soma zaidi »

BODI YA REA YAMPA SIKU 14 MKANDARASI WA UMEME MKOANI SIMIYU KUJIREKEBISHA

Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imempa siku 14 mkandarasi wa umeme vijijini mkoani Simiyu kuongeza kasi ya usambazaji umeme katika vijiji alivyopangiwa la sivyo Bodi hiyo haitasita kuchukua hatua mbalimbali za kimkataba ikiwemo ya kusitisha mkataba. Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Wakili Julius Kalolo  alisema hayo tarehe 16 …

Soma zaidi »

MKANDARASI WA UMEME WILAYANI CHATO ATEKELEZA MAAGIZO YA BODI YA REA

Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeeleza kuridhishwa kwake na utekelezaji wa maagizo iliyoyatoa kwa Mkandarasi anayefanya kazi ya kusambaza umeme vijijini wilayani Chato kampuni ya Whitecity Guangdong JV ambayo yalilenga kuongeza kasi ya usambazaji umeme vijijini. Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Wakili Julius Kalolo tarehe …

Soma zaidi »

KAMATI YA BUNGE YATOA MAONI KUHUSU MKATABA WA UMEME JUA

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wametoa maoni mbalimbali kwa Wizara ya Nishati, kuhusu kuanzishwa kwa ushirikiano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua (ISA). Walitoa maoni hayo Dodoma, Novemba 12, 2019 wakiwa ni sehemu ya wadau wa sekta husika ili kuboresha Mkataba huo kabla haujawasilishwa …

Soma zaidi »

HATUTAONGEZA MUDA – DKT KALEMANI

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amekataa maombi ya mkandarasi kampuni ya KEC International Ltd kutoka India, anayetekeleza mradi wa kupanua kituo cha kupoza umeme kilichopo Zuzu, mkoani Dodoma, kuongezewa miezi mitatu zaidi ili akamilishe kazi hiyo. Badala yake, Dkt Kalemani amemtaka Mkandarasi huyo kukamilisha kazi husika na kuikabidhi kabla …

Soma zaidi »

BODI YAWEKA KUSUDIO KUMFUTIA MKATABA MKANDARASI WA REA

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imeweka kusudio la kufuta mkataba mmojawapo wa mkandarasi anayetekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani Mtwara na sehemu ya Mkoa wa Tanga, ambaye ni muunganiko (JV) wa kampuni za Radi Services Ltd, Njarita Contractors Ltd & Aguila Contractors Ltd. Kusudio hilo liliwekwa bayana mbele ya waandishi …

Soma zaidi »

BODI YATOA TATHMINI KUHUSU UTEKELEZWAJI MIRADI YA UMEME VIJIJINI MOROGORO

Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Oktoba 25, mwaka huu ilikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Olesanare, taarifa ya tathmini kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo, baada ya ziara yao ya siku mbili. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Styden Rwebangila, …

Soma zaidi »