TANZANIA NA NAMIBIA WAJADILIANA KUHUSU SACREEE

  • Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Naibu Waziri wa Nishati wa Namibia, Kornelia Shilunga pamoja na ujumbe wake, wamekutana na kujadili kwa pamoja kuhusu Kituo cha Nishati Jadidifu na matumizi bora ya Nishati cha nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SACREEE).
  • Mgalu alikutana na ujumbe huo, Desemba 2, 2019, uliofika katika  Ofisi za Wizara  zilizopo jijini Dodoma, kwa lengo la kuisisitiza Tanzania kuweka saini katika  mkataba wa makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika( SADC) juu ya kuanzishwa kwa SACREEE.
2-01
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (Kushoto) akiongoza majadiliano ya pamoja na Ujumbe kutoka Namibia,(kushoto) na Watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati(kulia) kuhusu Kituo cha Nishati Jadidifu na matumizi bora ya Nishati cha nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SACREEE) katika Ofisi ya Wizara ya Nishati Dodoma.
  • Katika mazungumzo hayo, Mgalu aliueleza ujumbe huo kuwa  mpaka sasa Tanzania bado haijasaini Mkataba wa Makubaliano ya pamoja ya  utekelezaji wa kituo hicho hadi pale uamuzi wa kuanzishwa kwa kituo hicho utakapoidhinishwa na Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika( SADC).
  • Aidha, Mgalu alisema  baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria juu ya uanzishwaji wa SACREEE, Tanzania iko tayari kusaini mkataba kwa ajili kuwezesha kituo hicho ambacho Makao yake Makuu yako nchini Namibia.
3-01
Watendaji Wakuu wa Wizara ya Nishati wakiwa katika majadiliano ya pamoja ya Kituo cha Nishati Jadidifu na matumizi bora ya Nishati cha nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SACREEE) katika Ofisi ya Wizara ya Nishati Dodoma.
  • Halikadhalika, Mgalu alisema  kuwa Tanzania na Namibia ni nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ni dhahiri Kwamba nchi hizo zitakuwa zikishirikiana kwa namna moja ama nyingine katika masuala mengine mbalimbali kupitia umoja huo.
  • Sambamba na hilo alisema nchi hizo pia zinaweza kushirikiana kwa kuuziana umeme kupitia njia ya kusafirisha umeme wa kV400 inayojengwa kwa ajili ya kuunganisha gridi za Tanzania na Zambia(TAZA) kwakuwa nchi hizo ni wanachama wa Mtandao wa Southern Africa Power Pool (SAPP)ambao uko chini ya SADC.
4-01
Naibu Waziri wa Nishati wa Nambia, Kornelia Shilungwa,( kulia) akiwa na ujumbe alioambatana nao wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (hayupo pichani)wakati wamajadiliano ya pamoja ya Kituo cha Nishati Jadidifu na matumizi bora ya Nishati cha nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SACREEE) katika Ofisi ya Wizara ya Nishati Dodoma.
  • Kwa upande wake Naibu Waziri wa Namibia, Shilunga aliishauri kwamba  Tanzania isaini mkatba huo ili SARCEEE isonge mbele kwa manufaa nchi wanachama pia alisema Namibia inaendelea kuhamasisha nchi zilizobaki zisaini mkataba huo.
  • Tayari nchi 8 kati ya 16 zimekwisha kusaini Mkataba wa makubaliano ya pamoja ya nchi wanachama wa Jumuiaya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ya kuanzishwa kwa SACREEE ambayo ilizinduliwa mjini Windhoek nchini Namibia, Oktoba, 2018 na kuhudhuriwa na Mawaziri kutoka nchi wanachama wa SADC na Wakuu wa Taasisi za Kimataifa na Kikanda zinazohusika na sekta ya nishati. Na Zuena Msuya, Dodoma,
Ad

Unaweza kuangalia pia

TPDC YAOKOA TRILIONI 12.7 KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *