Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na baadhi ya walimu wa shule za sekondari katika halfa hiyo ya kukabidhi kompyuta 25 kwa shule 14 zilizopo katika halmashauri ya Kisarawe..(PICHA NA VICTOR MASANGU

WAZIRI JAFO AKABIDHI KOMPYUTA 25 KWA SHULE ZA SEKONDARI 14 KATIKA WILAYA YA KISARAWE

  • Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri nchini pamoja na maafisa elimu kuachana kabisa na vitendo vya kuwanyima fursa walimu ambao wanahitaji kujifunza somo la tehema na badala yake wahakikishe wanatoa vibali bila ya kuwa na ukilitimba wowote kwa lengo la kukuza teknolojia na mawasiliano.
  • Jafo ametoa kauli hiyo wakati wa halfa ya kukabidhi kompyuta 25 ambazo zimetolewa na serikali kupitia mfuko wa mawasilino kwa wote ambapo zitazinufaisha shule za sekondari 14 zilizopo katika halmashauri ya Kisarawe.
  • Jafo alibainisha kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawajengea uwezo walimu ambapo hadi sasa tayari walimu wapatao 570 wameshapatiwa mafunzo maalumu kwa ajili ya somo la tehema ili kuendana na kasi na mabadiliko ya kiteknolojia.
  • “Kitu kikubwa sisi kama serikali kwa sasa tumejipanga kuhakikisha kwamba somo hili la Tehama kwa walimu linapewa kipaumbele zaidi, lakini sipendi kuona walimu wananyimwa vibali kwa ajili ya kwenda kuongeza ujuzi katika somo hilo hivyo kuanzia sasa ofisi yangu italisimamia hili na kwamba wakurugenzi wote na maafisa elimu msiwanyime vibali kabisa wapeni acheni roho mbaya,”alisema Jafo.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kati kati akiwa ameshika moja ya kompyuta ambazo zmezitoa kwa niaba ya serikali, kushoto kwake ni Naibu waziri wa uchukuzi na Mawasialiano Injinia Atashasta Nditiye, na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo
  • Naye Naibu waziri wa uchukuzi na mawasiliano Injinia Atashasta Nditiye amesema kwamba kwa sasa serikali imeshaanza mchakato kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vituo 20 vya Tehama kwa upande wa Tanzania bara ambapo kwa upande wa Tanzania visiwani tayari wameshajenga vituo vya Tehama vipatavyo 10 ambavyo ni mahususi kwa wanafunzi, wanafanyakazi, pamoja na walimu.
  • Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema kwamba katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu wanatarajia kuanzisha kituo maalumu kwa ajili ya kufundishia somo la tehema kwa walimu pamoja na wanafunzi ili kuweza kupanua zaidi katika Nyanja ya teknolijia.
  • “Kwa kweli tunaishukuru sana serikali ya awamu ya tano kwa kutupatia vifaa hivi vya kompyuta 25 kwa ajili ya shule zetu za sekondari 14, bah ii itaweza kusaidia kwa kisi kikubwa kuongeza uwezo kwa walimu katika suala zima la teknolojia pamoja na mawasiliano,”alisema Jokate.
  • Komputa hizo 25 ambazo zimetolewa kwa shule 14 za Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani zimenunulia kwa kiasi ya shilingi milioni 43 zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa walimu pamoja na wanafunzi katika kusaidia suala zima la teknolojia pamoja na mawasiliano
Ad

Unaweza kuangalia pia

KINONDONI YA TUMIA BILIONI 1.5 UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *