TUMEDHAMIRIA KUONGEZA WIGO UPASUAJI – DKT. KAJUNGU

  • Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mkoani kilichopo mkoani Pwani katika Halmashuri ya Kibaha Mji Dkt. Godfrey Kajungu, amesema kuwa wamejizatiti kuongeza wigo wa utoaji wa huduma za upasuaji katika kituo hicho mara baada ya serikali kuwapatia Milioni 500 katika awamu tatu ya mpango wa serikali wa kuimarisha miundombinu ya Afya nchini.
  • Akizungumza muda mfupi mara baada ya Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima, Daktari Kajungu alisema kituo ca Afya cha mkoani ni moja vituo tegemeo katika Wilaya hiyo kutokana na kuhudumia wananchi zaidi 100 kwa siku wanaofika kwa matatizo mbalimbali ya kiafya.
  • “Kama mlivyosikia Naibu Katibu Mkuu ameagiza ndani ya wiki mbili jengo hili la upasuaji liwe limeanza kazi, sisi tunamthibitishia kuwa ifikapo tarehe 09 Februari, 2020 tutaanza shughuli za upasuaji katika jengo hili jipya ili kuwarahisishia wananchi huduma za afya.” Alisema Dkt. Kajungu.
111-01
Naibu Katibu Mkuu Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Dorothy Gwajima akiwa anakagua jengo jipya la upasuaji la Kituo cha Afya mkoani ambapo ametoa siku 14 kiwe kimeanza kazi. (Picha na OR-TAMISEMI)
  • Akizungumza mara baada ya kutembela majengo hayo mapya yaliyopokea milioni 500 mwezi Mei,2028 kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa baadhi ya huduma, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Dorothy Gwajima, aliutaka uongozi wa kituo hicho kuanza kutoa huduma hasa ikizingatiwa kuwa kituo hicho kipo umbali wa mita zisizozidi mita 400 hivyo uwepo wa huduma za upasuaji ni muhimu katika kuokoa maisha endapo dharura imetokea, lakini pia kituo hicho kwa sasa ndio kinatumika kama Hospitali ya Wilaya hadi hapo Hospitali ya Wilaya itakapo kamilika.
  • Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mganga mfawidhi wa kituo hicho, kituo cha Afya mkoani kina jumla ya Madaktari 9, madaktrari wasaidizi 4, Matabibu 4 na Maafisa wauguzi 3 Wauguzi wasaidizi 20, Wakunga 19 wataalamu wa maabara 10 na wataalamu wa Utrasound 2 idadi ambayo imetajwa kukidhi mahitaji  kwa sasa.
  • Naibu katibu mkuu yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi kukagua huduma za Afya, ikiwa ni muendelezo wa kuhakikisha katika kila kituo na Hospitali huduma za Afya zinatolewa kwa ubora ili wananchi waendelee kuvutiwa na kuendelea kuziamini Hospitali na Vituo hivyo kwani hali ya upatikanaji wa huduma kwa sasa imezidi kuboreshwa katika awamu hii ya tano. Na. Atley Kuni Kibaha- PWANI
Ad

Unaweza kuangalia pia

NAIBU WAZIRI SIMA – MIFUKO MBADALA ISIYOKIDHI VIWANGO MARUFUKU NCHINI

Serikali imesema kamwe haitaruhusu uzalishaji, uingizaji na matumizi ya mifuko mbadala aina ya Non-Woven isiyokidhi …

Oni moja

  1. такси эконом недорого https://taxi-vyzvat.ru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *