Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hawapo pichani) na viongoz wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa “Solidarity Forever” baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam

RAIS MAGUFULI AREJESHA UTARATIBU WA ZAMANI WA MALIPO YA WASTAAFU

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2018 ameagiza kurejeshwa kwa utaratibu wa ulipaji wa mafao ya wafanyakazi wanaostaafu uliokuwa ukitumika kabla ya kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii, na ametaka utaratibu huo utumike mpaka mwaka 2023 wakati wadau wakijadiliana juu ya kikokotoo kitakachotumika kulipa mafao hayo bila kuathiri mfuko na wastaafu kulipwa vizuri.
  • Mhe. Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo katika mkutano wake na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), vyama shiriki, viongozi wa mifuko ya hifadhi ya jamii (PSSSF na NSSF), Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).
Rais wa Jamhuri ya Muungano
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hawapo pichani) na viongoz wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa “Solidarity Forever” baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam
  • Katika mkutano huo Mhe. Rais Magufuli amesikiliza maoni ya viongozi hao kuhusiana na utekelezaji wa Sheria ya Mfuko ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma namba 2 ya mwaka 2018 na kanuni zake ambapo viongozi hao wameelezea changamoto zilizojitokeza kwa wastaafu kulipwa kiasi kidogo cha fedha za mafao ya mkupuo (25% badala ya 50% ya zamani), na taharuki iliyowakumba wafanyakazi ambao ni wastaafu wa baadaye.
  • Kabla ya kutangaza uamuzi huo Mhe. Rais Magufuli amesema uamuzi wa Serikali kuunganisha mifuko ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF na kuunda mfuko mmoja wa wafanyakazi wa Serikali uitwao PSSSF, na pia kuwa na mfuko mmoja wa wafanyakazi wa sekta binafsi uitwao NSSF ulitokana na mapendekezo ya wadau yaliyolenga kuondoa mkanganyiko wa kikokotoo cha mafao ya wastaafu na pia kuokoa baadhi ya mifuko iliyokuwa mbioni kufa kutokana na kuelemewa na madeni ya wastaafu.
Viongoz wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hawapo pichani) na viongoz wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa “Solidarity Forever” baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam .
  • Amebainisha kuwa katika kunusuru hali hiyo, Serikali ya Awamu ya Tano imelipa deni la makato ya wafanyakazi kwa mifuko ya hifadhi ya jamii la shilingi Trilioni 1.23 ambalo lilimbikizwa na pia imewalipa wastaafu waliokwama kulipwa mafao yao kiasi cha shilingi Bilioni 550 kati ya shilingi Bilioni 774 walizokuwa wakidai huku waliobaki wakiendelea kulipwa kadiri uhakiki unavyofanyika.
  • Hata hivyo amesema kufuatia hali ya sintofahamu iliyoibuka kutokana na kikokotoo cha mafao kilichotolewa baada ya kuanza kwa utekelezaji wa sheria mpya, Serikali haiko tayari kuona wafanyakazi wanakatishwa tamaa na haiko tayari kuona wastaafu wanapata shida baada ya utumishi mzuri kwa nchi yao, hivyo ameagiza urejeshwe utaratibu uliokuwa ukitumika kabla mabadiliko mpaka mwaka 2023 wadau watakapokubaliana utaratibu unaofaa kwa mifuko kuwepo na wafanyakazi kupata mafao mazuri.
KIKOKOTOO-3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hawapo pichani) na viongoz wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa “Solidarity Forever” baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam
  • “Serikali hii haipo hapa kukatisha tamaa wafanyakazi, wala haipo hapa kuwaumiza wastaafu, kustaafu sio dhambi na mtu anayestaafu anatakiwa kuheshimiwa kwa sababu katika utumishi wake amejitolea kulitumikia Taifa lake kwa moyo wake wote, ameingia kazini akiwa kijana anaondoka amezeeka” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipoongea na viongoz wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam.
  • Mhe. Rais Magufuli amesema katika kipindi cha mpito cha mpaka mwaka 2023 ambapo idadi ya wastaafu watakaolipwa mafao yao itakuwa 58,000 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na SSRA waisimamie vizuri mifuko ya hifadhi ya jamii ili iepukane na matumizi mabaya ya fedha, iboreshe daftari la wastaafu kwa kuondoa wastaafu hewa na ijiepushe na uwekezaji usiokuwa na tija, hali itakayoiwezesha kujiimarisha na kumudu kulipa mafao ya wafanyakazi ipasavyo.
  • Mkutano huo umehudhuriwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Dkt. Moses Kusiluka.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *