MKANDARASI JENGO LA WIZARA YA NISHATI ATAKIWA KUKAMILISHA KAZI YA UJENZI KWA WAKATI

  • Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amemtaka mkandarasi anayetekeleza kazi ya ujenzi wa Jengo la Wizara ya Nishati linalojengwa katika Mji wa Serikali, Ihumwa jijini Dodoma kuhakikisha kuwa anakamilisha kazi hiyo kwa wakati uliopangwa.
  • Akizungumza katika eneo la Ihumwa WaziriKalemani amesema kuwa, ili kufanikisha utekelezaji wa kazi hiyo kwa wakati ni vyema mkandarasi huyo ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akahakikisha kuwa vifaa vyote vinavyotakiwa katika kutekeleza kazi hiyo vinakuwepo katika eneo la kazi.
  • “Ni Lazima mkandarasi uhakikishe kuwa matofali, mchanga, simenti, mabati, kokoto, rangi, madirisha, nondo na vifaa vyote vinavyotakiwa hapa kwa ajili ya ujenzi vinapatikana kwa wakati wote katika eneo hili la ujenzi ili kuharakisha
    utekelezaji wa kazi hii kama ulivyopangwa na si vinginevyo”;
  • Akifafanua, Dkt. Kalemani amesema kuwa atakuwa akitembelea eneo hilo mara kwa mara kuona hatua za utekelezaji wa kazi hiyo na kuwaasa watendaji wa Wizara yake kuhakikisha kuwa wanafuatilia kwa karibu kazi husika ili itekelezwe kwa viwango vinavyotakiwa na kwa wakati.
  • Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hamisi Mwinyimvua amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa anaongeza mitambo inayotakiwa katika kutekeleza ujenzi huo ili kuongeza kasi ya utekelezaji.
  • Ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati ni utekelezaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Wizara zote kujenga majengo katika eneo hilo la Ihumwa unakojengwa mji wa Serikali unaojumuisha
    majengo ya Wizara zote.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SPIKA WA BUNGE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA WILAYA YA KONDOA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) leo azindua …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *