SPIKA WA BUNGE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA WILAYA YA KONDOA

M1-01
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (wa kwanza kushoto) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia ) leo wakipongezana baada ya kuzindua jengo jipya la kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Kondoa lililopo eneo la Kondoa Mjini. Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni George Mkuchika na wa pili kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria.
  • Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) leo azindua Jengo la kisasa lililojengwa kwa kutumia teknologia ya moladi Wilayani Kondoa
  • Akiwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Mahakama ya Wilaya ya Kondoa alisema miundo mbinu bora na ya kisasa katika muhimili wa Mahakama inawezesha mazingira tulivu ya uwekezaji na ukuaji wa biashara na hivyo kukuza Uchumi wa mtanzania na Taifa kwa ujumla wake.
  • Aidha, alisema anafarijika kwa niaba ya wanadodoma wote kuona upatikanaji wa majengo ya kisasa ya Mahakama kuanzia ngazi za mahakama za mwanzo hadi Wilayani.

M2-01
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Job Ndugai ( wanne kushoto) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa tatu kulia) wakikata utepe leo ikiwa ni ishara ya kuzindua jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Kondoa lililopo eneo la Kondoa Mjini. Wengine ni viongozi mbalimbali.
  • Pia, Mhe. Spika alisema Mifumo ya TEHAMA katika Mahaka ya kisasa kama hii itaboresha utoaji wa huduma za kimahakama na uharakishaji wa utoaji haki kwa wakati na kwa wote, aliwaomba Wananchi kutoa ushirikiano na chombo cha Mahakama kalinda na kutunza rasilima hiyo ya jengo kwani zimetumika fedha za ndani ambayo ni kodi za Wananchi.
  • Ili kutimiza adhima ya Mahakama Mh.Job aliahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kupitisha Bajeti zinazowasilishwa na Mahakama Bungeni ili kutoa fursa za kuendelea kuboresha Miundo mbinu ya Mahakama nchini alikiri kuwa takribani nchi nzima majengo ya mahakama ni mabovu na yaliyochakaa sana.
Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.