Pori kwa pori mbugani, Prof. Simon Msanjila akiongoza wajumbe walioambatana kujiridhisha, kukagua pamoja na kutoa kauli ya serikali kwa wafanya biashara wa madini wanaojihusisha na biashara hiyo kinyume na taratibu na sheria ya nchi, Nyuma yake mwenye suti ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani

SERIKALI INA MACHO – NAIBU WAZIRI BITEKO

  • Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewaeleza watanzania wasiofuata Sheria katika utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini nchini kuwa Serikali inaona na itafika popote madini yanapochibwa pasipo vibali halali vya kufanya shughuli hiyo.
  • Biteko ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, Tarehe 5 mwezi Januari, 2019 alipofanya ziara ya kukagua eneo ambako shughuli za uchimbaji wa madini ya shaba ulifanywa pasipo kibali na kubaini viashiria vya uchimbaji katika hifadhi ya Wanyama pori ya Makao iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.
Afisa Madini wa Mkoa wa Simiyu,
Afisa Madini wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Fredy Mahobe akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya ujumbe kutoka Wizara ya Madini, Mkuu wa Wilaya ya Meatu Joseph Eliaza Chilongani na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Meatu.
  • Akizungumzia lengo la ziara hiyo, Biteko alisema kumekuwa na viashiria vya kuwepo kwa watu wasiokuwa waaminifu na kujiingiza katika shughuli ya uchimbaji pasipokuwa na vibali jambo ambalo halikubaliki na halitavumilika. “Sisi madini yanatuuma, tukisikia kuna watu wanachimba tutafika mahali popote kujua madini hayo yanachimbwa na kupelekwa wapi” Biteko alikazia.
  • Aliendelea kwa kusema, huu mchezo ulifanyika sana na sasa nimekuja kuwaambia hautajirudia tena. Endapo mtu yeyote anataka kuchimba madini ya yoyote ikiwa ni pamoja na madini ya ujenzi kama vile mchanga wa kutengenezea barabara sharti afike katika ofisi zetu za madini aeleze nia na eneo analotakiwa kutengeneza barabara na wahusika watamuonesha eneo la kuchimba mchanga kwa utaratibu wa kisheria kwa matumizi hayo si kujiamlia tu.
NAIBU-4
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani akiongea jambo mara baada ya kupokea ugeni kutoka Wizara ya Madini katika wilaya yake ya Meatu
  • Biteko alisisitiza kuwa lengo la ziara hiyo si kutoa kibali kwa watu kuchimba katika hifadhi hiyo. “Sisi hatujaja kupromote watu wachimbe bali tumekuja kwa sababu watu wanachimba pasipo taratibu.
  • Alibainisha kuwa ili mtu yeyote apate kibali cha kuchimba katika hifadhi hiyo sharti apate kibali kutoka mamlaka kuu nne ambazo ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji kwa sababu katika hifadhi hiyo kuna vyanzo vya maji, Mamlaka ya Mazingira (NEMC)pamoja na Wizara ya Madini.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wakwanza kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila na wajumbe aliambatana nao wakiwa katika eneo linaloonesha dalili za uchimbaji wa madini katikati ya hifadhi ya wanyama ya Makao wilayani Meatu
  • Katika ziara hiyo ya kushtukiza Biteko aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila aliyeelezea sheria na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili mtu yeyote kuweza kujihusisha na shughuli za Madini.
  • Aidha, Profesa Msanjila aliwataka watanzania kujua kuwa rasilimali madini zinazopatikana nchini ni kwa manufaa ya watanzania wote hivyo ni lazima wafuate utaratibu ili mapato yatokanayo na tozo mbalimbali kutokana na utafiti, uchimbaji na biashara ya madini ziwanufaishe watanzania wote. “Lazima niwaambie haya madini ni ya watanzania wote” alikazia.
  • Akizungumzia chanzo cha taarifa ya kuwepo kwa uchimbaji katika hifadhi hiyo Leons Welenseile (Mjiolojia) alisema mnamo mwaka 2016 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alifanya ziara iliyolenga kutatua mgogoro baina ya kampuni ya inayomiliki leseni ya uwindaji wanyamapori katika hifadhi hiyo Mwiba Holdings Limited na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo baada ya wananchi kutoridhishwa na kile walichokuwa wakikipata kutoka kwa mwekezaji huyo.
Baadhi ya wanyama
Baadhi ya wanyama wanaoonekana katika hifadhi ya wanyama ya Makao katika Wilaya ya Meatu Mkoani Singida
  • Walipokuwa njiani kutoka katika kusuluhisha mgogoro huo ndipo wataalamu wa madini katika mkoa huo walikutana na loli lililobeba mchanga pasipokuwa na vibali halali vya kufanya uchimbaji huo nakubaini kuwa shughuli hiyo ilikuwa ikifanywa na kampuni hiyo ya mwiba kwa lengo la kukarabati barabara katika hifadhi hiyo pasipo kujua kuwa walipaswa kuwa na leseni ya kuchimba mchanga huo na kupigiwa hesabu iliyopelekea kulipa mrabaha wa milioni 50 baada ya kukiri kufanya shughuli hiyo kwa muda mrefu.
  • Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani alikiri kutokuwa na taarifa za uchimbaji huo na kuwataka wataalamu na maafisa madini katika eneo lake kutoa taarifa pindi masuala ya ukiukwaji wa taratibu na sheria za nchi yanapotokea katika eneo lake ili kuweza kushirikiana katika kutatua changamoto hizo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

UCHUMI WA TANZANIA WAZIDI KUKUA NA KUIMARIKA

Hali ya uchumi wa Tanzania yazidi kuimarika na kukua  kwa asilimia 6.9 ikiwa ni  takwimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *